top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

7 Aprili 2020 18:55:22

Clindamycin

Clindamycin

Ni antibiotiki iliyo kwenye kundi la lincosamide inayotumika kutibu maambukizi makali ya bakteria wanaouliwa na dawa hii pamoja na kutibu chunusi za vulgarizi. Kemikali ya lincosamide huvunwa kutoka kwa bakteria anayeitwa Streptomyces lincolnensis.


Clindamycin hutibu bakteria aina ya anaerobiki pamoja na gram- chanya cocci na bacilli and gram-hasi bacilli. Kwa kushangaza dawa hii pia inaonekana kuua baadhi ya protozoa na imekuwa ikitumika mbali na matumizi yake iliyoelekewa, ili kutibu toksoplasmosis, maleria na babesiosisi.


Clindamycin huvunjwa na Ini kabla ya kutolewa mwilini, Figo na mfumo wachakula huhusika kusafisha dawa hii kwa kuitoa nje ya mwili.


Fomu na uzito wa dawa ya Clindamycin


  • Dawa ya clindamycin hupatikana kwenye mfumo wa tembe, majimaji ya kuchoma sindano au ya kuwekewa kwenye mishipa ya damu. Dawa hii huwa na uzito wa

  • 150-300mg kwa Kidonge

  • 2ml ( 150mg/ml) kwa dawa ya Sindano

  • 10g kwa krimu au jeli


Bakteria wanaouliwa na Clindamycin

Baadhi ya bakteria ambaowanauliwa na Dawa hii huwa Ni bacteria jamii ya


  • Staphylococci

  • Streptococci

  • Pneumococci


Magonjwa yanayotibiwa na Clindamycin


Dawa Clindamycin hutibu magonjwa yafuatayo

  • Kutibu magonjwa ya ngozi na tishu laini

  • Kutibu magonjwa ya mfumo wa upumuaji njia ya juu mfano neumonia

  • Kutibu maambukizi katika mfumo wa uzazi kwa wanawake

  • Kutibu mifupa na maungio

  • Kutibu maambukizi ya uti wa mgongo

  • Kutibu magonjwa ya kuambukiza yaliosababishwa na vimelea ( septicaemia)


Maudhi ya matumizi ya Clindamycin


Baadhi ya maudhi madogo madogo ya Dawa Ni pamoja na;

  • Kuharisha

  • Kutapika

  • Kuwashwa ngozi

  • Kupata Upele( rashes)

  • Homa

  • Maumivu ya tumbo

  • Mwili kuwa na uchovu

  • Maumivu ya kichwa

  • Misuli kuuma

  • Kukosa hamu ya chakula

  • Kupata manjano katika macho, ngozi

  • Kushindwa kupumua vizuri

  • Maumivu ya kifua

  • Kuhisi kizunguzungu

  • Ngozi kuvimba na kupata uwekundu


Dawa zisizopaswa kutumika na Clindamycin


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kwa sababu madhara makubwa yanaweza kutokea zikitumika kwa pamoja;

  • Chanjo hai ya BCG

  • Chanjo ya kipindupindu

  • Erythromycin

  • Chanjo hai ya Typhoid

  • Cisatracurium

  • Onabotulinumtoxina

  • Pancuronium

  • Rapacuronium

  • Rimabotulinumtoxinb

  • Rocuronium

  • Succinylcholine

  • Vecuronium

  • Atracurium


Angalizo kwa watumiaji wa Clindamycin


Tumia Dawa hii kwa Umakini kwa wagonjwa hawa;

  • Wenye shida ya Ini

  • Wenye shida ya Figo

  • Kwa mama wajawazito na wanao nyonyesha

  • Wazee

  • Wenye historia ya kua na pumu(asthma)

  • Wenye matatizo ya mzio kwenye ngozi( kama pumu ya ngozi- eczema)


Matumizi ya Clindamycin wakati wa ujauzito


Dawa hii itumiwewakati wa ujauzito endapo faida zinazidi hasara.


Matumizi ya Clindamycin Wakati wa kunyonyesha


Dawa hii hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, dawa kwa mtoto anayenyonya huwa na madhara kiasi kama kuharisha, maambukizi ya kandida na mara chache damu kwneye kinyesi, damu kwenye kinyesi huwa ni dalili ya kolaitizi inayosababishwa na hii dawa.


Endapo umesahau dozi Clindamycin ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi kwenye muda uliopangiwa, tumia dawa hiyo mara utakapokumbuka. Ruka dozi uliyosahau endapo muda wa kutumia dozi nyinginr umekaribia sana.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:49:08

Rejea za mada hii:-

1.Clindamycin Uses, dosage, Warnings at https://www.drugs.com/clindamycin.html. Imechukuliwa 6.4.2020

2.Clindamycin Dosage,Uses, Warning , Side effects at https://www.webmd.com/drugs/2/drug-12235/clindamycin-hcl-oral/detaiols. Imechukuliwa 6.4.2020

3.Clindamycin Uses,dosage, interaction s, Side effects at https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682399.html. Imechukuliwa 6.4.2020

4.Clindamycin information on Uses, Dosage, Interaction, warning, Side effects at https://www.rxlist.com/clindamycin-drug.htm. Imechukuliwa 6.4.2020

5. Drugs.com. Clindamycin.https://www.drugs.com/clindamycin.html. Imechukuliwa 07.04.2020

6. Drugbank. Clindamycin.https://www.drugbank.ca/drugs/DB01190. Imechukuliwa 06.04.2020
bottom of page