Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Aprili 2020, 13:06:16

Dapsone
Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu ukoma- (antileprosi), dawa hii hutumika kwa pamoja na rifampicin na clofazimine ili kutibu ukoma. Dawa hii inayojulikana kwa jina jingine la diaminodiphenyl sulfone, hupatikana katika mfumo wa kidonge na jeli ya kupaka, kidonge huwa na uzito wa 25mg au 100mg.
Jinsi Dapsone inavyofanya kazi
Humzuia bakteria kuzalisha foliki asidi. Foliki asidi ni muhimu sana kwenye seli ya bakteria kwani inahusika katika utengenezajiwa wa protini mbalimbali na Jinomu ya bakteria, inapozuia bakteria hushindwa kujizalia na wengine hufa.
Dawa hii hutumika kumlenga bakteria wa ukoma mwenye jina la mycobacterium leprae, lakini pia inaweza kutumika pamja na pyrimethamine kutibu malaria.
Kazi za dawa ya Dapsone
Hutumika kutibu ugonjwa wa Ngozi wa Demataitizi Hepatiformizi
Hutumiwa na dawa zingine kutibu ugonjwa wa ukoma
Hutumika kama kinga ya kuepusha kupata nimonia inayosababishwa na pneumocystis (karinii) Jiroveci
Hutumika kwa wagonjwa wenye kinga ya chini kuwalinda kutopata ugonjwa wa toksoplasmosisi.
Huweza kutumika kutibu malaria ikitumiwa Pamoja na pyrimethamine
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Dapsone
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :
Aluminum hydroxide
Apalutamide
Chanjo hai ya BCG
Calcium carbonate
Famotidine
Ibuprofen
Idelalisib
Ivosidenib
Lansoprazole
Mefloquine
Nefazodone
Sodium bicarbonate
Sodium citrate
Chanjo hai ya typhoid
Voxelotor
Tahadhari ya Dapsone kwa wagonjwa wafuatao;
Tahadhari ya dawa hii
Hupelekea kupungua kwa kiasi cha chembechembe nyeupe za damu
Chukua tahadhari unapomtibu mgonjwa mwenye mzio na kemikali ya sulphonamide.
Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye mzio na dawa hii
Matumizi ya Dapsone Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Kwa mama anayenyonyesha haipaswi kutumika
Maudhi ya Dapsone
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;
Agranyulosaitosisi
Upungua hamu ya kula
Kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu
Anemia ya hemolitiki
Maumivu ya kichwa
Madhaifu ya Ini
Haipoalbuminemia
Kukosa usingizi
Mzio wa lepra
Methaemoglobinemia
Kupoteza kazi mota
Kichefuchefu
Nyuropathi ya mfumo wa fahamu wa pembeni
Mzio mkali wa ngozi
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Kutapika
Je endapo umesahau dozi ya Dapsone ufanyeje?
Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dozi anapaswa kuitumia pale atakapokumbuka
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:46:40
Rejea za mada hii:-