Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
Imeboreshwa:
24 Januari 2026, 16:48:23

Dawa Cotrimoxazole
Cotrimoxazole ni dawa ya kuua vimelea (antibayotiki) inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa dawa mbili: Sulfamethoxazole na Trimethoprim. Hutumika kutibu maambukizi mbalimbali ya bakteria kwenye mfumo wa upumuaji, mkojo, tumbo, ngozi, pamoja na magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa wenye kinga dhaifu kama wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Majina ya kibiashara
Cotrimoxazole hujulikana pia kwa majina yafuatayo ya kibiashara:
Septrin
Bactrim
Cotrim
Cotrim Forte
Septrin DS
Cotrimoxazole ipo kundi gani la dawa?
Cotrimoxazole ipo katika makundi yafuatayo ya dawa:
Antibiotiki
Sulfonamides
Antifolate combination antibiotics
Dawa zilizo kundi moja na Cotrimoxazole
Sulfamethoxazole
Trimethoprim
Sulfadiazine
Sulfasalazine
Sulfisoxazole
Fomu za Cotrimoxazole
Dawa hii hupatikana katika fomu zifuatazo:
Kidonge (tablet)
Syrup (kwa watoto)
Injection (katika mazingira ya hospitali)
Uzito wa Cotrimoxazole
Kidonge:
400 mg Sulfamethoxazole + 80 mg Trimethoprim
800 mg Sulfamethoxazole + 160 mg Trimethoprim (DS – Double Strength)
Sirapu:
200 mg Sulfamethoxazole + 40 mg Trimethoprim kwa 5 ml
Cotrimoxazole hutibu nini?
Cotrimoxazole hutumika kutibu:
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
Kuharisha kunakosababishwa na bakteria
Maambukizi ya mfumo wa upumuaji
Nimonia aina ya Pneumocystis jirovecii
Maambukizi ya ngozi na tishu laini
Homa ya matumbo (typhoid – kwa baadhi ya mazingira)
Maambukizi ya masikio (otitis media)
Kinga (prophylaxis) kwa wagonjwa wanaoishi na VVU
Namna Cotrimoxazole inavyofanya kazi
Cotrimoxazole hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa folic asid ndani ya bakteria. Mchanganyiko wa Sulfamethoxazole na Trimethoprim huzuia hatua mbili tofauti za mchakato wa folate, jambo linalosababisha bakteria kushindwa kuzaliana na hatimaye kufa.
Binadamu hupata folate kutoka kwenye chakula, hivyo huathirika kidogo ikilinganishwa na bakteria.
Ufyozwaji wa Cotrimoxazole
Hufyonzwa vizuri kupitia mfumo wa chakula
Hufikia kiwango cha juu kwenye damu ndani ya masaa 1–4
Husambazwa vizuri kwenye mapafu, mkojo, ngozi na maji ya ubongo
Mwingiliano wa Cotrimoxazole na chakula
Inaweza kutumika pamoja au bila chakula.Hata hivyo, kuitumia pamoja na chakula hupunguza maudhi ya tumbo kama kichefuchefu.
Mwingiliano wa Cotrimoxazole na pombe
Ingawa si marufuku kabisa, inashauriwa kuepuka pombe wakati wa kutumia Cotrimoxazole kwa sababu:
Huongeza maudhi ya tumbo
Huongeza hatari ya kizunguzungu
Huongeza mzigo kwa ini
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cotrimoxazole
Wenye mzio wa Sulfonamides
Wagonjwa wenye historia ya Stevens-Johnson syndrome
Wagonjwa wenye upungufu mkali wa ini au figo
Watoto wachanga chini ya wiki 6
Wagonjwa wenye upungufu wa G6PD (tahadhari kali)
Utoaji taka wa Cotrimoxazole mwilini
Hutolewa zaidi kupitia mkojo
Sehemu hutolewa kama dawa halisi na nyingine kama mazao ya umetaboli
Wagonjwa wenye figo dhaifu huhitaji kupunguziwa dozi
Matumizi ya Cotrimoxazole kwa mama mjamzito
Cotrimoxazole haishauriwi sana katika trimester ya kwanza kwa sababu inaweza kuathiri ukuaji wa neva wa mtoto kutokana na kuzuia folate.Inaweza kuzingatiwa katika mazingira maalum endapo faida ni kubwa kuliko hatari.
Matumizi ya Cotrimoxazole kwa mama anayenyonyesha
Kiasi kidogo hupita kwenye maziwa ya mama.Kwa ujumla ni salama kwa watoto wakubwa, lakini tahadhari inahitajika kwa watoto wachanga au wenye homa ya manjano.
Dawa zenye mwingiliano mkali na Cotrimoxazole
Warfarin
Phenytoin
Methotrexate
ACE inhibitors (hatari ya hyperkalemia)
Cyclosporine
Maudhi madogo ya Cotrimoxazole
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Upele wa ngozi
Maumivu ya kichwa
Kukosa hamu ya kula
Maudhi makubwa (nadra lakini hatari)
Sindromu ya Stevens-Johnson
Ugonjwa mkali wa kuoza kwa ngozi ya juu (epidemis)
Kupungua kwa chembe damu
Hepataitis
Kushindwa kwa figo
Ufanye nini kama umesahau dozi yako?
Kama umesahau dozi:
Tumia mara tu unapokumbuka
Ikiwa muda wa dozi inayofuata umekaribia, ruka dozi uliyosahau
Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa:
24 Januari 2026, 16:48:23
Rejea za mada hii:-
