top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

Imeboreshwa:

24 Januari 2026, 04:27:29

Dawa Promethazine

Dawa Promethazine

Promethazine ni dawa Gani?

Promethazine ni dawa ya kundi la phenothiazine ambayo hutumika kama:

  • Antihistamine: kupunguza dalili za mzio/aleji (kifua, koo, ngozi)

  • Dawa ya kuzuia kutapika kupunguza kichefuchefu na kutapika

  • Dawa ya usingizi: kusaidia usingizi kwa wagonjwa wenye hofu au wasi wasi

  • Dawa ya kuzuia kikohozi: kupunguza kikohozi kikavu


Promethazine inaweza kutumika peke yake au kama sehemu ya mchanganyiko na dawa nyingine, kama vile kwa sitapu ya kikohozi.


Fomu za Promethazine zinazopatikana

  • Vidonge / Tableti: 10–25 mg

  • Sirapu: 5 mg/5 mL au 6.25 mg/5 mL

  • Sindano: ya misuli (IM) au mishipa ya damu (IV) kwa uangalizi wa hospitali

Sindano inapaswa kutolewa tu na mtaalamu wa afya, kwa sababu inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa itumike vibaya.

Majina Mengine ya Promethazine

  • Phenergan

  • Fargan

  • Phenadoz

  • Promethazine HCl


Matumizi ya Promethazine

  1. Mzio na kuumuka ngozi (wekundu, kuvimba, na vipele)

  2. Kichefuchefu na kutapika (kemotherapi, upasuaji, au msafara)

  3. Kikohozi kikavu na homa

  4. Usingizi kwa wagonjwa wenye wasiwasi au usingizi hafifu

  5. Homa ya safari(kutapika safarini) (kichefuchefu kinachotokana na usafiri)


Maudhi / Madhara ya Promethazine


Maudhi ya kawaida
  • Usingizi / fatigue

  • Kizunguzungu / kichwa kuzunguka

  • Kinywa kikausha

  • Haja ngumu (constipation)

  • Kutapika / kichefuchefu kidogo


Maudhi makubwa (Hatarishi)
  • Kupumua polepole au kushuka kwa shinikizo la damu

  • Kutegemea dawa (uraibu wa dawa), hasa kwa matumizi ya muda mrefu)

  • Degedege au kuongezeka kwa hasira

  • Matatizo ya mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo- Nadra (Arithimia)

  • Neuroleptic malignant syndrome (ndani ya hospitali, hatari sana)


Tahadhari muhimu

  • Wazee na wagonjwa wa moyo, figo au ini wanapaswa kutumia kwa uangalifu

  • Epuka pombe au dawa za usingizi wakati unatumia Promethazine

  • Hujapendekezwa kwa wagonjwa wenye historia ya presha kwenye macho (glaukoma)


Katazo (Marufuku)

  • Usitumie kwa watoto chini ya miaka 2

  • Wagonjwa wenye historia ya mzio kwa Promethazine au phenothiazines nyingine

  • Wagonjwa wenye upungufu mkali wa kupumua

  • Wagonjwa walio kwenye hatari ya kushuka shinikizo la damu kubwa


Matumizi wakati wa ujauzito na Kunyonyesha


Ujauzito
  • Hata ingawa tafiti ndogo zinaonyesha kuwa Promethazine inaweza kutumika kwa ujauzito wa awali, hakupendekezwi sana katika miezi ya mwisho

  • Sababu: inaweza kusababisha usingizi mkubwa kwa mtoto mchanga au matatizo ya kupumua


Kunyonyesha
  • Dawa hii hupita kwenye maziwa ya mama

  • Huweza kusababisha usingizi kwa mtoto

  • Matumizi yanapaswa kuwa kwa uangalizi wa daktari, na faida lazima iwe kubwa kuliko hatari


Endapo umesahau kunywa Dozi

  • Kunywa dozi mara tu unapokumbuka

  • Ikiwa muda wa dozi inayofuata umekaribia, ruka dozi uliyosahau

  • Usiongeze dozi ili kufidia uliyosahau


Muhtasari

Promethazine ni antihistamine na antitussive inayotumika kupunguza allergy, kichefuchefu, na kikohozi kikavu, lakini inaweza kusababisha usingizi mkali na madhara makubwa kwa watoto, wajawazito, na wanaonyonyesha.Inapaswa kutumika tu chini ya uangalizi wa daktari na kwa dozi sahihi.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara na majibu yake

1. Je, Promethazine inafaa kwa watoto wadogo?

Hapana, si salama kwa watoto chini ya miaka 2 kutokana na hatari ya kupumua kushuka na maudhi makali.

2. Je, inaweza kusababisha utegemezi?

Ndiyo, hasa iwapo itumike kwa muda mrefu kama sedative. Matumizi ya muda mfupi kwa madhumuni maalum yameonekana kuwa salama.

3. Inatibu kikohozi chenye makohozi?

Hapana. Promethazine hutumika zaidi kwa kikohozi kikavu, si kikohozi chenye makohozi mengi.

4. Je, inafaa kwa kichefuchefu cha usafiri?

Ndiyo, huweza kupunguza motion sickness, lakini haifai kwa watoto wadogo.

5. Je, inaweza kutumika kwa homa?

Inafaa kama sehemu ya dawa ya kupunguza kikohozi na homa, lakini haiwezi kutibu sababu ya homa yenyewe (kama maambukizi).

6. Je, inaweza kuongezwa na pombe?

Hapana. Kunywa pombe pamoja kunaongeza hatari ya usingizi mkali, kupumua polepole na kushuka shinikizo la damu.

7. Nini madhara makubwa zaidi?

  • Kupumua polepole

  • Kushuka kwa shinikizo la damu

  • Mapigo ya moyo kwenda isivyo kawaida (Arithimia)

  • Sindromu ya dalili hatari za mfumo wa fahamu (Neuroleptic malignant syndrome) hutokea mara chache lakini ina hatari kubwa ya kutishia uhai wa mtu.

8. Inaathirije ujauzito?

Matumizi ya miezi ya mwanzo yanaonekana kuwa salama kidogo, lakini miezi ya mwisho hairuhusiwi bila ushauri wa daktari.

9. Inaathirije kunyonyesha?

Huenda ikasababisha usingizi kwa mtoto, hivyo matumizi lazima yafanyike kwa angalizi wa kitabibu.

10. Je, inaweza kuchanganywa na antihistamine nyingine?

Hapana, inaongeza madhara ya usingizi na kizunguzungu, hivyo lazima iangalizwe na daktari.


ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

24 Januari 2026, 04:04:28

Rejea za mada hii:-

Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 13th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2018.

Katzung BG, Trevor AJ. Basic & Clinical Pharmacology. 15th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2021.

Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020.

World Health Organization. WHO Model Formulary. Geneva: World Health Organization; 2019.

U.S. Food and Drug Administration. Promethazine Drug Safety Communication. Silver Spring (MD): FDA; 2020.

Rang HP, Ritter JM, Flower RJ, Henderson G. Rang and Dale’s Pharmacology. 9th ed. London: Elsevier; 2020.

Wong A, Robinson P. Antihistamines in allergy and cough management: Promethazine review. J Clin Pharm Ther. 2019;44(3):423–432.
bottom of page