Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 10:44:54
Dawa ya Bificonazole
Bificonazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa Imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Canesten.
Fomu ya dawa na wingi wa kiini
Bificonazole hupatikana pia katika fomu ya krimu yenye kiini cha dawa asilimia 1
Namna Bificonazole inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuharibu kizuizi cha upenyezaji kwenye seli ya fangasi. Dawa hii husababisha kuzuia utengenezaji wa egosteroli, ambayo ni sehemu muhimu ya seli ya fangasi.
Dawa zilizo kundi moja na Bificonazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
• Butoconazole • Clotrimazole • Econazole • Fenticonazole • Isoconazole • Ketoconazole • Luliconazole • Omoconazole • Oxiconazole • Sertaconazole • Sulconazole • Tioconazole
Kazi ya Bificonazole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhari ya kuchukua kwa watumiaji wa Bificonazole
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao:
• Wagonjwa wenye aleji na dawa nyingine za antifangasi
Utofauti wa Bificonazole na dawa zingine za Imidazole
Dawa hii Nusu ya maisha yake ni masaa 1-2
Matumizi ya Bificonazole wakati wa ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Bificonazole wakati wa kunyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi kwa mtumiaji wa Bificonazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na; • Kupata vipele • Kuhisi kuungua • Maumivu ya tumbo • Kuwashwa mwili
Ukisahau kutumia dozi ya Bificonazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-