Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020, 05:44:04
Dawa ya Cephalexin
Cephalexin ni aina ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la kwanza la antibayotiki jamii ya Cephalosporin. Dawa hii hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Keflex na Panixine Disperdose
Rangi na Fomu ya Cephalexin
Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza Cephalexin hupatikana katika mfumo wa tembe,maji na kidonge wenye uzito wa milligramu zzifuatazo: Tembe
• 250 mg • 500 mg • 750 mg
Maji
• 125 mg/5mL • 250 mg/5mL
Kidonge
• 250 mg • 500 mg
Namna cephalexin inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria
Dawa kundi moja na Cephalexin
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja la Cephalosporin daraja la kwanza ni ; • Cefazolin • Cefadroxil • Cephalothin • Cephapirin • Cephradine
Kazi ya cephalexin
• Hutumika kwenye matibabu ya tezi kuvimba • Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye pharyngitis • Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ya mfumo wa mkojo • Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi kwenye sikio
Utofauti wa Cephalexin na dawa zingine kwenye kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la cephalosporin ya kwanza; • Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni nusu saa mpaka saa 1 tangu itumike mwilini
Dawa usizopaswsa kutumia pamoja na Cephalexin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :
• Argatroban • Bivalirudin • Dalteparin • Enoxaparin • Fondaparinux • Heparin • Warfarin • Bazedoxifene • Dienogest • Estradiol • Ethinylestradiol • Probenecid
Wagonjwa wasiopasswa kutumia Cephalexin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin
Tahadhari ya Cephalexin
• Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo • Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili
Matumizi ya Cephalexin kwa mama mjamzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito • Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito ,Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Matumizi ya Cephalexin kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya Cephalexin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Maumivu ya tumbo • Kichefuchefu • Kutapika • Kuharisha • Homa
Ukisahau kunywa dozi ya Cephalexin
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-