Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
7 Julai 2020 20:00:13
Dawa ya Ketoconazole
Ketoconazole ni dawa jamii ya antifangasi inayotumika kukinga na kutibu maradhi yanayosababishwa na fangasi.
Majina mengine ya ketoconazole
Hufahaika pia kama; • Nizoral
Fomu na uzito wa ketoconazole
Ketoconazole hupatikana katika fmu ya kidonge chenye uzito wa; • 200mg Ketoconazole hupatikana pia katika fomu ya krimu yenye ujazo mbalimbali
Namna ketoconazole inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng’enya cha saitokromu P-450 ambacho ni muhimu inayohusika kuzalisha homoni ya ergosteroli kutoka kwenye kiungo lanosteroli. Homoni hii huwa muhimu katika ukuta wa seli za fangasi, kukosekana kwa homoni hii katika kuta hufanya kuta hizo kuwa dhaifu na fangasi hufa.
Ketoconazole hutibu nini?
Ketoconazole jutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi kama; • Fangasi wa vidole vya miguu (athlete's foot) • Vibarango • Aina kadhaa za mba • Pityriasis (tinea versicolor) • Blastomycosis • Fangasi ukeni • Coccidioidomycosis • Histoplasmosis • Chromomycosis • Paracoccidioidomycosis
Matumizi nje ya kazi yake
Hutumika kwenye matibabu ya sindromu ya Cushing's inayotokana na madhaifu ya ndani ya mwili
Ufyonzaji na utoaji taka mwilini wa ketoconazole
• Ufyonzaji wake huwa mzuri wkenye mazingira ya utindikali • Utumiaji na chakula hupunguza ufyonzaji wake( ingawa ni kinyume na maandiko mbalimbali) • Asilimia 76 ya dawa huweza kufyonzwa na kuingia mwilini Asilimia 2 hadi 4 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo, asilimi 95 ya dawa huondolewa mwilini kwa kufanyiwa umetaboli na ini
Dawa zilizo kundi moja na Ketoconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo; • Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Econazole • Fluconazole • Flucytosine • Griseofulvin • Itraconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole
Dawa zisizopaswa kutumika na Ketoconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Alfuzosin • Alprazolam • Cobimetinib • Conivaptan • Dihydroergotamine • Disopyramide • Dronedarone • Eliglustat • Flibanserin • Ibutilide • Indapamide • Isoniazid • Ivabradine • Lomitapide • Lovastatin • Lurasidone • Methadone • Naloxegol • Nisoldipine • Pentamidine • Pimozide • Procainamide • Quinidine • Ranolazine • Regorafenib • Simvastatin • Sirolimus • Sotalol • Triazolam • Venetoclax • Ziprasidone
Wagonjwa wasiopaswakutumia ketoconazole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao: • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi • Wagonjwa wenye Magonjwa ya Ini
Upekee wa ketoconazole
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni Dawa hii huwa na madhara mengi ya mfumo wa tumbo(gastrointestino)na kuleta hepataitizi inayotegemea dozi- kwa sasa ni njema kutumia kama dawa ya kupata ili kuepuka madhara yake.huwa ni nzuri zaidi ukilinganisha na dawa ya miconazole na clotrimazole kwa sababu huwa na uwanja mpana wa kuua fangasi na hufyonzwa vema Dawa hii humeng'enywa na Ini na pia hutolewa mwili kwa njia ya Ini kwa asilimia 95 na asilimia 2-4% n kwa njia ya mkojo. Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa mawili mpaka masaa nane kwenye mwili.
Matumizi ya ketoconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya ketoconazole wakati wa kunyonyesha
Takwimu zinaonyesha kuwa, kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mama na kumfikia mtoto hivyo haishauriwi itumike kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Ketoconazole
Baadhi ya maudhi ya dawa hii ni pamoja na : • Kichefuchefu • Kutapika • Maumivu ya tumbo na kichwa • Kizunguzungu • Kupata Homa • Kuharisha • Kukosa hamu ya tendo la ndoa • Mwili kuwa manjano • Kuogopa mwanga • Kuwashwa mwili
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa au \paka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-