Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020 11:15:44
Dolutegravir
Dawa hii huuzwa katika kwa jina la Tivicay, Dolutegravir ni aina ya dawa mojawapo za kudhibiti maambukizi ya VVU. Dawa hii hutumika ikiwa imeungana na dawa zingine za kudhibiti maambukizi ya VVU-ARTs Dolutegravir imeanza kutumika karibuni hapa Tanzania na ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la Integrase inhibita- INSTI INSTI hufanya kazi kwa kuzuia kimeng’enya cha intagrase ambaye huzuia kipindi cha mpito (Intergration) kutoka kwenye DNA iliyotengenezwa inayoelekea kwenye DNA ya kirusi ,Hivyo dawa hii huzuia hii hatua isifanikiwe. Dawa hii husaidia kupunguza HIV mwilini ili kinga ya mwili iweze kuwa vizuri.
Fomu uzito na rangi ya Dolutegravir
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge. Rangi yake ni ya njano, hata hivyo inategemea rangi iliyopendekezwa na kampuni.
Dolutegravir inaruhusiwa kutumikana chakula?
Huweza kutumika pamoja au pasipo na chakula bila kujalisha kama ni chakula cha mafuta au sio.
Dawa zilizo kundi moja na Dolutegravir
Dawa nyingine ambayo ipo kwenye kundi moja na Dolutegravir(DTG) ni :
Raltegravir
Kazi za Dolutegravir
Kazi za Dolutegravir(DTG) ni kama zifuatazo:
Hutolewa pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV kuzuia Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya mama kujifungua
Muunganiko wa dawa ya Dolutegravir
Dolutegravir hutumika kama muunganiko wa kwanza katika kuthibiti virusi vya HIV pamoja na muunganiko wa dawa zifuatazo ;
Tenofovir (TDF) +Lamivudine (3TC) + Dolutegravir (DTG)
Tenofovir (TDF) +Lamivudine (3TC)+Dolutegravir (DTG)
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Dolutegravir
Dolutegravir haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Dofetilide
Carbamezapine
Efavirenz
Nevirapine
Phenytoin
Phenorbabitol
Rigampin
Tipranavir
Etravirin
Dolutegravir itumike kwa umakini kwa kina nani?
Inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa wa:
Aliyewahi kuwa na mzio wa dawa hii
Aliyewahi kuwa na ugonjwa wa ini ni kama homa ya Ini
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Dolutegravir
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao :
Wenye aleji na dawa hii
Haipaswi kutumika pamoja na dofetilide
Matumizi ya Dolutegravir Kwa mama mjamzito
Hutumika kwa mama mjamzito kwa ajili ya kuzuia na kupunguza Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hivyo matokeo ya dawa hukabiliwa na kuthibitiwa kwa shida yeyote itakayojitokeza.
Matumizi ya Dolutegravir Kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote.
Maudhi ya matumizi ya Dolutegravir
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:
Kuchoka
Kuwa na sukari ya juu
Kukosa usingizi
Maumivu ya misuli
Kuchoka
Maumivu ya kichwa
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Ndoto zisizo za kawaida
Kuongeza kolestro mwilini na kumpelekea mtu kuwa kunenepa
Huweza kusababisha oma ya ini
Je endapo utasahau dozi yako ya Dolutegravir ufanyaje?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti VVU. Endapo utasahau kunywa dozi kwenye muda uliopangiwa unapaswa kunywa mara utakapokumbuka. Endapo muda umekaribia wa kunywa dozi nyingine basi subiria muda ufike na unywe dozi hiyo kama ulivyopangiwa na daktari wako.
Endapo una wasiwasi basi wasiliana na Daktari wako kwa maelezo zaidi
Mambo muhimu kujua kuhusu dawa ya Dolutegravir
Dawa ya Dolutegravir inaweza kusababisha mzio mkali wa kutishia uhai wa mtu. Inaweza kuhusisha mzio wa haipasensitiviti na matatizo ya figo
Tahadhari kwa mtumiaji wa Dolutegravir
Wasiliana na mhudumu wako wa afya mara moja endapo unapata harara wakati unatumia dawa hii. Acha kutumia dawa hii endapo unapata harara inayoambatana na dalili zilizotajwa hapa chini.
Homa
Kujihisi mwili unaumwa
Kuchoka
Maumivu ya misuli au maungio ya mwili
Kuota malenge ya maji
Macho kuwa na rangi nyekundu au ngozi
Kupata shida ya kupumuao lipsi na ulimi
Kupata shida ya kupumua
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:36:00
Rejea za mada hii:-