Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Aprili 2020 13:29:19
Doravirine
Doravirine ni dawa ya kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI iliyo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NNRTIs.
Dawa jamii ya NNRTIs hufanya kazi kwa kuzuia kimengenya cha kirusi kinachoitwa Reverse Transkriptezi. Kimen’enya hiki kikizuiwa kufanya kazi, huzuia kirusi cha UKIMWI kujizalia Zaidi, na hivyo kupunguza idadi ya virusi vya UKIMWI mwilini. Idadi ya virusi vya UKIMWI vinapopungua mwilini husababisha kinga ya mwili kutoharibika na kuwa imara Zaidi.
Fomu na Rangi ya Doravirine
Dawa huuzwa katika jina la Pifeltro na hutumika pamoja na dawa zingine ili kuwa na nguvu Zaidi.
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge
Rangi yake hutegemea mzalishaji wa dawa, baadhi ya dawa zina rangi ya njano.
Huweza kutumika Pamoja/ bila chakula
Dawa zilizo kundi moja na Doravirine
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Doravirine ni zifuatazo;
Nevirapine (NVP)
Etravirine(ETR)
Efavirenz
Baadhi ya dozi zinazoungana na dawa hii ni;
Doravirine + lamivudine + tenofovir disoproxil fumarate)
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Doravirine
Doravirine haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amorbabital
Apalutamide
Bosentan
Carbemezapine
Efavirenz
Clobazam
Etravirine
Mitotane
Phenytoin
Phenobarbital
Rifampin
Tahadhari ya Doravirine kwa wagonjwa wafuatao
Magonjwa mengine yanayoharibu kinga ya mwili kama Graves disease
Matumizi ya Doravirine Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Matumizi ya doravirine Kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha bado hakuna madhara yaliyojitokeza kwa mama mjamzito na mtoto
Matumizi ya doravirine kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote ili kuzuia usugu wa kirusi kwenye dawa hii kwa mtoto.
Maudhi ya Doravirine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kizunguzungu
Kukosa usingizi
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kuchoka
Maumivu ya kichwa
Je endapo umesahau dozi ya Doravirine ufanyeje?
Endapo utasahau kunywa dozi yako, kunywa mara moja unapokumbuka. Endapo muda wa kunywa dozi ingine umefika, usitumie bali endelea na dozi kama kawaida na ruka dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:36:11
Rejea za mada hii:-