top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

22 Aprili 2020 18:55:20

Dulaglutide

Dulaglutide

Dulaglutide ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linalojulikana kama Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Trulicity hupatikana kwenye mfumo wa maji na hutumika kwa kuchoma sindano chini kidogo ya Ngozi.


Unapotumia dawa hii unapaswa kuwa umekula chakula ili kuepuka madhara ya kushuka sana kwa kiwango cha sukari kwenye damu.


Hakikisha unachoma Sindano kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Choma sindano hii kwenye mapaja, tumbo au sehemu ya juu ya mkono kama Daktari atakavyokuelekeza, ni vyema kubadili badili eneo la kuchoma sindano kwenye ngozi ili kuepuka kama kuvimba kwenye ngozi


Dulaglutide, hupatikana kwenye uzito wa miligramu


  • 0.75mg/0.5mL

  • 1.5mg/0.5mL


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Dulaglutide


  • Liraglutide

  • Taspoglutide

  • Lixisenatide

  • Semaglutide


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine kwenye kundi hili la (GlP1 Inhibita):


Dulaglutide inauwezo mdogo wa kuthibiti sukari ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili hasa GlP1 Inhibita.


Namna inavyofanya kazi;


Hufanya kazi ya kuchochea tezi kongosho kuzalisha homoni ya Insulin, hufanya kazi endapo kiwango cha sukari ni kikubwa kwenye damu.


Homoni ya Insulin husaidia seli za mwili zitumie sukari na kuhifadhi katika ini sukari inayozidi. homoni ya insulin inapozalishwa kwa wingi kutokana na shinikizo la dawah ii hupelekea kiwango cha sukari kupungua kwenye damu.


Dulaglutide hutibu nini?


Hutumika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili.


Inashauriwa pia kutumika kupunguza hatari kubwa yaa magonjwa ya moyo(mshituko wa moyo, infaksheni ya mayokadia, na kiharusi) kwa wagonjwa wa kisukari aina ya 2


Dawa zisizopaswa kutumiaka na Dulaglutide


Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;

  • Warfarin

  • Valproic acid

  • Tolbutamide

  • Tolazamide

  • Theophylline

  • Tacrolimus

  • Sitagliptin

  • Sirolimus

  • Saxagliptin

  • Rosiglitazone

  • Repaglinide

  • Quinine

  • Quinidine

  • Procainamide

  • Primidone

  • Prazosin

  • Pramlintide

  • Pioglitazone

  • Phenytoin

  • Phenobarbital

  • Nateglinide

  • Minoxidil

  • Miglitol

  • Metformin

  • Lithium

  • Linagliptin

  • Levothyroxine

  • Insulin glulisine

  • Insulin glargine

  • Insulin detemir

  • Insulin degludec

  • Insulin aspart

  • Glyburide

  • Glipizide

  • Glimepiride

  • Fosphenytoin

  • Ethosuximide

  • Empagliflozin

  • Disopyramide

  • Digoxin

  • Dapagliflozin

  • Cyclosporine

  • Clonidine

  • Chlorpropamide

  • Carbamazepine

  • Canagliflozin

  • Alogliptin

  • Acarbose


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao


Wagonjwa wenye mzio na dawa hii


Kwa wagonjwa wenye saratani ya tezi thairoidi au kuwa na historia ya saratani hii kwandugu wat umbo moja.


Tahadhari ya matumizi ya Dulaglutide


  • Endapo itatumika na dawa homoni ya Insulin hushusha zaidi kiwango cha sukari kwenye damu.

  • Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya 1

  • Huleta Hatari ya kupata pancreataitizi

  • Huleta hatari ya figo kuferi


Matumizi ya Dulaglutide mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi B3 la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito kutokana na makundi yaliyowekwa na shirika la dawa Australia. Shirika la dawa ulimwenguni bado halijaweka dawa hii kwenye makundi ya dawa salama kipindi cha ujauzito.


Matumizi ya Dulaglutide kwa mama anayenyonyesha


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito na kwa mama anayenyonyesha


Maudhi ya Dulaglutide


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


  • Kichefuchefu

  • Mwili kuchoka

  • Kuharisha

  • Kutapika

  • Maumivu ya tumbo

  • Kukosa hamu ya kula


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau dozi yako, tumia pale unapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umefika. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana kufika acha dozi uliyosahau kisha endelea na dozi kama ulivyopangiwa na daktarin wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:34:02

Rejea za mada hii:-

1.Medscape.Dulaglutide.https://reference.medscape.com/drug/trulicity-dulaglutide-999965. Imechukuliwa 22/4/2020

2.WebMd.Dulaglutide.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-167024/dulaglutide-subcutaneous/details. Imechukuliwa 22/4/2020

3.MedlinePlus.Dulaglutide.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a614047.html. Imechukuliwa 22/4/2020

4.Drugs.Dulaglutide.https://www.drugs.com/mtm/dulaglutide.html. Imechukuliwa 22/4/2020
bottom of page