Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Aprili 2020, 08:00:24

Fenoprofen
Fenoprofen ni dawa ya kutuliza maumivu makali ya mwili kwa kuzuia uzalishaji wa homoni ya prostaglandini.Dawa hii hupatikana kutoka jamii ya NSAIDS. Hupatikana mfumo wa vidonge na tembe.
Dawa hii hufanya kazi yake ya kwa kuzuia uzalishwaji wa prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa husababisha homa Pamoja na uvimbe kwenye sehemu ya mwili yenye tatizo.
Umeetaboli wa Fenoprofen
Umetaboli wa fenoprofen hufanyika kwenye Ini na Utoaji taka mwili kupitia Figo Kwa njia ya mkojo na kinyesi
Fomu na uzito wa Fenoprofen
Fenoprofen Inapatikana fomu na uzito ufuatao;
Kidonge chenyemilligramu 600mg
Tembe yenye miligramu 200 na 400
Fenoprofen hutibu nini?
Kupunguza uvimbe kutokana na majeraha
Homa
Kupunguza maumivu
Kutibu arthraitis
Kutibu osteoarthraitis
Angalizo
Fenoprofen inatakiwa kutolewa kwa Umakini kwa watu wenye magonjwa
Wenye matatizo ya Moyo, kiharusi
Wenye shida ya Ini
Wenye shida ya Figo.
Wenye historia ya Pumu (asthma)
Wenye mzio au mzio na dawa jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen
Dawa mwiko kutumika na Fenoprofen
Fenoprofen hairuhusiwi kutumika pamoja na
Usitumie Dawa hii pamoja na dawa jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen, naproxen hii hupelekea hatari ya kupata vidonda vya tumbo
Usitumie Dawa hii pamoja na dawa zinazoyeyusha damu mfano warfarin
Usitumie Dawa hii pamoja na dawa jamii ya diuretic mfano Furosemide
Usitumie Dawa hii pamoja na dawa Captopril, Lisinopril kundi la dawa ACE inhibitors
Usitumie dawa hii pamoja na dawa ya Lithium
Usitumie dawa hii pamoja na dawa ya Methotrexate
Matumizi ya Fenoprofen kwa Wajawazito
Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi ya mwanzoni na miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.
Matumizi ya Fenoprofen kwa Wanaonyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Ukisahau dose Nini kifanyike
Kama umesaau kutumia Fenoprofen unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, acha dozi uliyoruka na kunywa dozi ingine kwa muda uliopangiwa na daktari wako.​
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:32:56
Rejea za mada hii:-