Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020, 19:00:43
Folate
Neno foleti ni neno tiba la ulyclinic limetumika kumaanisha neno tiba folate
Foleti ni nini?
Ni aina ya vitamin B9 ambayo hupatikana kwenye vyakula. Madini haya huwa hayatengenezwi mwilini, hupatikana kwa kula vyakula vyenye Folate kwa wingi tu.
Folate kabla ya kuingia kwenye damu, mfumo wa chakula huibadilisha na kuwa Vitamin B9
Mwili wako unahitaji folate ili uweze kutengeneza vinasaba. Madini haya ni muhimu sana kwa mama na mtoto akiwa tumboni. Madini ya folati huzuia hatari ya kupata upungufu wa damu na endapo itatumika mapema katika miezi ya kwanza au kabla ya kupata ujauzito husaidia kufanyika vema kwa mfumo wa fahamu wa mtoto hivyo kuzuia dhidi ya magonjwa ya mfumo wa fahamu mfano mgongo wazi na tundu kwenye Uti wa mgongo.
Mwili pia unahitaji foleti ili seli ziweze kujizalia na kuponyamwili unapopata majeraha.
Vyakula vyenye Foleti kwa wingi
Kunde
Maharagwe
Mayai
Mboga za majani kama Spinachi
Matunda kama Machungwa,Limau na zabibu
Ini la Ng'ombe
Papai
Ndizi
Parachichi
Madhara ya Upungufu wa foleti
Huongeza kwa kasi kiwango cha kemikali ya homocysteine inayopelekea hatari ya kupata magonjwa ya moyo
Kuzaliwa watoto walemavu endapo itakosekana kwa mama mjamzito
Hatari ya kupata saratani endapo Foleti itashuka
Upungufu wa damu mwilini
Kazi za madini Folate mwilini
Kutengeneza vinasaba (DNA)
Kufanya matengenezo ya DNA yenye shida
Kuzalisha chembechembe nyekundu za damu
Dalili za upungufu wa folate
Dalili za mtu mwenye upungufu wa folate
Uchovu wa mwili
Nywele kubadilika rangi
Kupata vidonda mdomoni
Ulimi kuvimba
Matatizo ya ukuaji kwa mtoto
Dalili za upungufu wa damu wa folate
Dalili za mtu mwenye upungufu wa damu kutokana na upungufu wa foleti
Uchovu wa mwili
Udhaifu
Kuwa na ngozi nyeupe
Shida ya kupumua
Kutokujisikia vizuri
Mapigo ya moyo kwenda haraka na
Dalili zingine za upungufu wa damu mwilini
Visababishi vya upungufu wa Folate mwilini
Vyakula tunavyokula, ukila vyakula ambavyo si vya matunda kwa wingi.
Kupika chakula kwa muda mrefu hupunguza madini haya
Magonjwa yanayoathiri mfumo wat umbo na ufyozwaji wa madini kama aina mbalimbali za saratani ,Ugonjwa wa Crohn, magonjwa sugu ya figo.
Hali ya kurithi. Watu wengine wana mfumo wa vinasaba ambao unashindwa kubadili foleti kuwa kwenye mfumo rahisi ili itumike mwilini.
Matumizi ya dawa ya phenytoin, methotrexate,sulfasalazine
Kunywa pombe kwa wingi
Vipimo kwa mtu mwenye upungufu wa folate
Ili kujua upungufu wa foleti mwilini kipimo cha mkojo huchukuliwa ili kupima kiwango cha madini haya
Nini madhara ya upungufu wa Madini ya Foleti ?
Kupata anemia ya meganoblastic:Ni upungufu wa damu ambao hutokana na upungufu wa foleti. Chembechembe nyekundi za damu huwa kubwa Zaidi na kushindwa kufanya ipasavyo kutokana na kukosa madini haya.
Hupelekea kiasi kidogo cha chembechembe nyeupe, pletileti
Hupelekea ulemavu wa kuzaliwa kwa Watoto kama mgongo wazi n.k
Matibabu ya upungufu wa madini Folate
Kula vyakula vyenye wingi wa madini ya foleti
Kupata madini ya foliki acid kwa wingi kama dawa ya ziada
Wale wenye magonjwa ya kurithi yanayoathiri ufyonzwaji wa madini haya wanapaswa kutumia folate yenye methyl
Mama mjamzito anapaswa kuepuka pombe ili kuepuka upungufu wa madini haya.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:33:16
Rejea za mada hii:-