Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Aprili 2020 18:04:38
Gliquidone
Gliquidone ni dawa mojawapo inayotumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kisukari iliyo kwenye kundi la sulfonylurea kizazi cha pili. Dawa hii inaweza kusababisha mgonjwa akakojoa mara kwa mara.
Majina ya kibiashara ya Gliquidone
Glurenorm
Beglynor
Gliquidonum
Fomula ya kikemikali
Fomu ay kikemikali ya Gliquidone ni C27H33N3O6S
Jina la kisayansi (IUPAC)
Gliquidone hufahamika kama 1-cyclohexyl-3-[4-[2-(7-methoxy-4,4-dimethyl-1,3-dioxoisoquinolin-2-yl)ethyl]phenyl]sulfonylurea
Namna ya kutumia Gliquidone
Meza kama ulivyo elekezwa na daktari wako.
Dawa hii huweza kutumika pamoja na dawa nyingine kama vile metformin kama akipendekeza daktari wako.
Dawa za kushusha sukari hutumika sambamba na lishe Pamoja na mazoezi sahihi kwa wagonjwa wa kisukari.
Ufanyaji kazi wa Gliquidone
Inachochea seli beta za kongosho kuzalisha insulini ambayo ndiyo hushusha sukari ya damu.
Inapunguza kasi ya ini kutengeneza sukari.
Muingiliano na dawa zingine
Dawa zinazoongeza ufanisi wa gliquidone;
Chloramphenicol
Clofibrate
Fluconazole
Methyldopa
Isocarboxazid
Phenelzine
Tranylcypromine
Choline salicylate
Diflunisal
Magnesium salicylate
Salsalate
Sodium salicylate
Sodium thiosalicylate
Sulfamethizole
Sulfamethoxazole
Sulfasalazine
Sulfisoxazole
Trimethoprim
Trimethoprim–sulfamethoxazole
Trisulfapyrimidine
Trovafloxacin
Dawa zinazo punguza ufanisi wa Gliquidone
Vidonge vya uzazi wa mpango
Amlodipine
Bepridil
Diltiazem
Nicardipine
Nifedipine
Verapamil
betamethasone
budesonide
dexamethasone
Dexone,
hydrocortisone
sodium phosphate
Nani asiyepaswa kutumia Gliquidone
Marufuku kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na kemikali zenye salfa.
Wagonjwa wa wa kisukari aina ya kwanza
Maudhi madogo ya Gliquidone
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Kichefuchefu
Kuwashwa ngozi
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Madhara makubwa ya Gliquidone
Sukari kushuka kupita kiasi
Kupoteza fahamu
Mzio mkali wa sindromu ya Steven Johnson
Matumizi ya Gliquidone wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Ni vyema kuepuka kutumia dawa hii wakati wa ujauzito na kunyonyesha kwani hakuna taarifa za kutosha juu ya madhara yake wakati wa ujauzito au wakati wa kunyonyesha. Dawa nyingine zinazopendekezwa na mamlaka za afya kama vile insulin zinaweza kutumika.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:33:45
Rejea za mada hii:-