Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Aprili 2020, 16:26:15
Golimumab
Golimumab ni dawa mojawapo inayotumika
Majina ya kibiashara
Golimumab huuzwa kwa jina la Simponi
Fomu ya dawa
Golimumab hupatikana katika fomu ya kimiminika kinachotolewa kwa kuchomwa sindano.
Kundi la dawa Golimumab
Golimumab ipo kwenye kundi la cytokine modulator
Dawa kundi moja na Golimumab
Dawa zingine katika kundi la cytokine modulator ni,
Infliximab
Adalimumab
Dawa hizi zimetengenezwa kutoka kwenye antibodi za monokrono, antibodi hizi hufanya kazi za kuzuia uamshwaji wa chembe hai zinazohusika katika kuamsha michomo kinga ambazo ni tumor necrotic factor alfa.
Ni sehemu yoyote unapata Golimumab
Golimumab inatakiwa kutumika chini ya uangalizi maalumu kutoka kwa mtaalamu mbobezi wa dawa. Hivyo huwezi ipata sehemu yoyote.
Golimumab na chakula
Haina madhara yeyote ya muingiliano na chakula
Jinsi Golimumab inavyofanya kazi
Golimumab hushambulia Tumor necrosis factor alfa (TNF). TNF huzalishwa na mfumo wa kinga yenye kazi ya kuamsha mwitikio wa mfumo wa kinga unaopelekea michomo na uharibifu wa maungio ya mwili.
Golimumab licha ya kutokuwepo kwenye makundi ya dawa za maumiv, inauwezo wa kupunguza maumivu ya maungio ya mwili.
Golimumab hutibu nini?
Hutumika kwa wagonjwa wa Ryeumatoid arthraitizi (baridi yabisi)
Hutumika kwa wagonjwa wa psoriatic arthritis ,Ni aina ya arthritis ambayo huathiri watu wenye matatizo ya ngozi
Hutumika kwa wagonjwa wenye aksio spondailoarthraitizi ,hii ni aina ya arthraitizi ambayo dalili moja kuu ya mgonjwa ni maumivu ya mgongo
Hutumika kwa wagonjwa wa ankailozing spondilaitizi ,hii ni aina ya arthraitizi ambayo huathiri zaidi uti wa mgongo na jointi kubwa za mwili
Hutumika kwa wagonjwa wa juvinaili idiopathiki arthraitizi ,hii ni aina ya arthraitizi ambayo hupelekea kuvimba kwa jointi zaidi ya moja hasa hasa huathiri wadada katika umri wa shuleni.
Hutumika kwa wagonjwa wa asaletivu colaitizi
Matumizi ya golimumab na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :
Chanjo ya Anthrax
Chanjo ya BCG
Chanjo ya tetenusi
Chanjo ya hepatitis A
Chanjo ya hepatitis B
Chanjo ya influenza
Chanjo ya surua
Chanjoo ya kichaa cha mbwa
Chanjo ya tetekuwanga
Chanjo ya virusi vya varicelle
Chanjo ya virusi vya zoster
Chanjo ya pneumokoka
Chanjo ya tetekuwanga
Chanjo ya rubella
Chanjo ya rota
Adalimumab
Alefacept
Anakinra
Azathioprine
Antithymocyte globulin equine
Antithymocyte globulin rabbit
Azathioprine
Baricitinib
Basiliximab
Canakinumab
Certolizumab pegol
Cyclosporine
Etanercept
Everolimus
Glatiramer
Hydroxychloroquine sulfate
Infliximab
Leflunomide
Mycophenolate
Rilonacept
Sirolimus
Tacrolimus
Temsirolimus
Tocilizumab
Tongkat ali
Chanjo ya taifodi
Chanjo hai ya taifodi
Ustekinumab
Vedolizumab
Angalizo la golimumab
Tahadhari ya Golimumab kwa wagonjwa wafuatao;
Huweza kuongeza hatari ya kupata Maambukizi zaidi sababu hupunguza kinga ya mwili
Huweza kupelekea hatari ya moyo kutokufanya kazi
Hupunguza chembechembe nyeupe za danu
Kama mgonjwa atapata hali ya lupasi dawa hizi zinapaswa kusimamishwa ,hali hii ni uvimbe ambao
hutokea endapo seli za kinga ya mwili zitashambulia zenyewe
Huweza kupelekea shida kwenye ini
Golimumab na ujauzito
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito
Pia haitumiki kwa wagonjwa wenye Maambukizi ya VVU , saratani, kifua kikuu na wenye matatizo ya mapafu na moyo
Golimumab kipindi cha kunyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika mama anapokuwa kipindi cha kunyonyesha.
Maudhi ya Golimumab
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
Kuharisha
Chakula kutokumeng'enywa vizuri
Kizunguzungu
Udhaifu wa misuli
Maumivu ya kichwa
Kupanda kwa hhinikizo la damu
Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji
Kupata maumivu au uvimbe kwenye sehemu ya sindano
Mashambulizi ya fangasi
Mashambulizi ya virusi kama Influenza
Je, kama umesahau dozi ya Golimumab ufanyeje?
Kama ukisahau kutumia dozi yako,wasiliana na daktari kwa maelekezo zaidi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:31:10
Rejea za mada hii:-