top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

25 Juni 2020 18:37:09

Indapamide

Indapamide

Utangulizi


Ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na kuondoa uvimbe unaotokana na kuvia kwa maji kwenye chemeb za mwili . Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa za Thiazide Diuretics


Dawa hii huwa maarafu kwa majina ya Microzide,HydroDiuril, Hydro na Esidrix


Rangi ya dawa huweza kuwa nyeupe ,lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza


Dawa hii haina madhara inapotumika pamoja na chakula


Indapamide hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa;


• 1.25 Mg

• 2.5 Mg


Namna dawa inavyofanya kazi


• Hufanya kazi kwa kuzuia ufyozwaji wa madini ya Sodiamu kloraidi na maji kwenye mirija ya figo hivyo kupelekea mtu kukojoa mara kwa mara

• Ufyozwaji wa maji unapozuiwa hurusu maji mengi kwenye mwili kupungua na hivyo kupunguza uvimbe wa miguu kuvimba kwa wagonjwa wa moyo


Madini ya Sodiamu yanapopungua mwilini huzuia mishipa ya damu kubana na hivyo huruhusu hupanuka na kushusha shinikizo la damu


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;


• Bendroflumethiazide

• Chlorothiazide

• Methyclothiazide

• Polythiazide

• Hydrochlorothiazide

• Metolazone


Kazi ya dawa ;


• Hutumika kutibu hali ya kuvimba kwa sehemu za mwili kama miguu na uso ambayo hali hii huweza kuwatokea wagonjwa walioferi moyo na wagonjwa wa ini na figo

• Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu



Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


• Amitriptyline

• Amoxapine

• Artemether/lumefantrine

• Chlorpromazine

• Clomipramine

• Desipramine

• Disopyramide

• Dofetilide

• Doxepin

• Dronedarone

• Droperidol

• Epinephrine

• Erythromycin base

• Fluconazole

• Fluphenazine

• Haloperidol

• Ibutilide

• Imipramine

• Ketoconazole

• Lofepramine

• Maprotiline

• Moxifloxacin

• Nilotinib

• Nortriptyline

• Octreotide

• Pentamidine

• Perphenazine

• Pimozide

• Procainamide

• Pochlorperazine

• Promazine

• Promethazine

• Protriptyline

• Quinidine

• Sotalol

• Thioridazine

• Trazodone

• Trifluoperazine

• Trimipramine

• Ziprasidone


Tahadhari ya dawa hii

• Inatumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wa kisukari,wenye upungufu wa Electrolyte,wenye kalisiamu kwa wingi ,wenye shinikizo la chini la damu

• Hupaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wa figo na ini

• Ina hatari ya kupunguza uwezo wa mwanaume katika mapenzi


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao ;


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii

• Wagonjwa Wenye shida ya kukojoa


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito pamoja na mama anayenyonyesha



Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;


• Shinikizo la damu kuwa chini

• Mapigo ya moyo kusikika kusiko kawaida

• Kizunguzungu

• Maumivu ya kichwa

• Kuchoka

• Kukosa hamu ya kula

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Kukojoa sana

• Kutokuona vizuri

• Elekrolaiti kupungua

• Vipele


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?


Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dawa anapaswa kutumia pindi anapokumbuka isipokuwa endapo muda wa kunywa dozi nyngine umefika, ruka dozi uliyoisahau kasha endelea na dozi kwa mud aulipangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman’s The pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 ukurasa wa 769

2.WebMd.Indapamide.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-12360/indapamide-oral/details. Imechukuliwa 25/6/2020

3.MedScape.Indapamide.https://reference.medscape.com/drug/indapamide-342415. Imechukuliwa 25/6/2020

4.NHS.Indapamide.https://www.nhs.uk/medicines/indapamide/. Imechukuliwa 25/6/2020
bottom of page