top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Aprili 2020 04:27:07

Indomethacin

Indomethacin

Ni dawa jamii ya NSAIDs, hutumika kupunguza maumivu makali, kupunguza uvimbe kutokana na majeraha na kukakamaa kwa maungio ya mwili kutokana na ugonjwa wa athraitizi, gauti, bazaitizi na tendinaitizi inflamesheni


Fomu na Uzito


Dawa hii hupatikana kwa mfumo wa tembe, unga kwa ajili ya kuchoma na majimaji ya kunywa. Huweza kuitwa majina mbalimbali ya kibiashara kama Indocin n.k


Metabolizimu ya dawa hufanywa na Ini, utoaji wa dawa mwilini hufanywa na Figo pamoja na mfumo wa chakula. Hivyo dawa hutoka mwilini kwa njia ya mkojo na kinyesi.


Dawa hii huweza kuishi mwilini kwa kiwango cha kupunguza maumivu kwa masaa ma nne na nusu tu.


Hupatikana kwa Tembe milligramu 25-50mg


Matumizi ya indomethacin


Dawa ya Indomethacin hutibu


• Kutibu maumivu makali ya mwili mfano maungio ya miguu na mikono

• Kutibu maumivu ya osteoathraitizi

• Kutibu arthraitisi ya rheumatoid ( baridi yabisi)

• Kutibu gauti

• Maumivu ya miguu kwa wagonjwa wa kisukari

• Kutibu maumivu ya mabega yanayosababishwa na burzaitizi/ tendinaitisi

• Kutibu maumivu ya mgongo na miguu


Maudhi madogo madogo ya Dawa


• Kizunguzungu

• Maumivu ya kichwa

• Kichefuchefu na kutapika

• Kuharisha

• Kupata kiungulia

• Maumivu ya tumbo

• Kuvimbiwa

• Kushindwa kupumua vizuri

• Maumivu ya kifua

• Upele katika ngozi

• Uchovu wa mwili

• Kuvimba uso


Tahadhari ya Indomethacin


Tumia Dawa hii kwa umakini kwa wagonjwa hawa


• Wenye shida ya moyo sababu inaweza kuongeza shinikizo la damu, kupelekea kiharusi

• Wenye shida ya Pumu ya kifua(asthma)

• Wenye shida ya Ini

• Wenye shida ya Figo

• Wenye mzio mkali

• Kuepukika katika hatua za mwisho za ujauzigo

• Haitolewi kwa yeyote mwenye Umri chini ya miaka 14


Dawa zisizopaswa kutumika na indomethacin


Dawa hii hairuhusiwi kutumika pamoja na


• Benazepril

• Captopril

• Lisinopril

• Methotrexate

• Tacrolimus

• Perindopril

• Quinapril

• Ramipril

• probenecid

• Aminolevulinic

• Apixaban

• Enalapril

• Erdafitinib

• Fosinopril

• Ketorolac

• Macimorelin

• Methyl aminolevulinate

• Moexipril

• Pemetrexed

• Siponimod

• Trandolapril

• antidiprizantsi


Indomethacine na ujauzito na Wanaonyonyesha


Epuka kutumia Dawa hii katika ujauzito miezi 3 ya mwisho maana inadhuru mtoto alieko tumboni


Indomethacin na unyonyeshaji


Dawa ya Indomethacin inaruhisiwa kwa mama anaenyonyesha Sababu ya kiwango kidogo cha Indomethacin kuingia katika maziwa ya mama wakati wa kunyonyesha.


Je, ufanye nini ukisahau dose ya Indomethacin


Kama umesaau kunywa dose yako Unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika Unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:31:59

Rejea za mada hii:-

1.Indomethacin Uses, side effects and Interactions at https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8880-5186/indomethacin-oral/indomethacin-oral/details. Imechukuliwa 8.4.2020

2.Indomethacin Uses, side effects and warnings at https://www.drugs.com/mtm/indomethacin.html. Imechukuliwa 8.4.2020

3.Indomethacin Uses, dosage and side effects at https://www.rxlist.com/indocin-drug.htm. Imechukuliwa 8.4.2020

4.Drugbank. Indomethacin. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00328. Imechukuliwa 8.4.2020
bottom of page