Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Mei 2025, 11:33:49
Insulin NPH
Insulin NPH (Neutral Protamine Hagedorn) ni aina ya insulini ya muda wa kati inayotumika kutibu na kudhibiti sukari ya damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya 1 na aina ya 2. Ni insulini iliyochanganywa na protamine ambayo huongeza muda wa kuanza na kudumu kwa athari za insulini mwilini.
Majina mengine ya Insulin NPH
Humulin N (Eli Lilly)
Novolin N (Novo Nordisk)
Uzito na fomu ya Insulin NPH
Sindano (pen) 100 units/mL
Chupa (vial) 10 mL
Dawa kundi moja na Insulin NPH
Insulin isophane (kundi la insulini za muda wa kati)
Insulin lente (inafanana na NPH lakini haitumiki sana leo)
Insulin NPH hutibu Nini?
Kisukari aina ya 1
Kisukari aina ya 2 kinapohitaji insulini
Kudhibiti sukari kwa muda mrefu mwilini
Namna Insulin NPH Inavyofanya kazi
Insulin NPH huanza kufanya kazi ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya kuchomwa na hufikia kilele chake ndani ya masaa 4 hadi 12. Athari zake hudumu kwa masaa 12 hadi 16, hivyo hutumika mara mbili kwa siku kwa kawaida kwa kudhibiti sukari ya damu kwa muda mrefu.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Insulin NPH
Wenye mzio wa insulini au viambato vyake
Wagonjwa wenye hypoglycemia kali
Wagonjwa wenye athari mbaya kali za insulini awali
Ufyonzwaji wa Insulin NPH
Insulin NPH hufyonzwa polepole kutokana na protamine iliyochanganywa, ikitoa athari ya polepole na kudumu zaidi.
Umetaboli Insulin NPH
Insulin NPH hubadilishwa na enzymes mwilini kuwa viambato visivyo na shughuli za insulini.
Matumizi ya Insulin NPH kwa Mama Mjamzito
Matumizi ya insulini NPH yanachukuliwa kuwa salama wakati wa ujauzito na hutumika kwa udhibiti wa kisukari kwa wanawake wajawazito kwa ushauri wa daktari.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Insulin NPH ni salama kwa mama anayetumia na kunyonyesha, bila madhara kwa mtoto.
Mwingiliano wa Insulin NPH na Dawa Nyingine
Beta-blockers: huweza kuficha dalili za hypoglycemia
Diuretics na corticosteroids: huongeza sukari damu
Pombe: huongeza hatari ya hypoglycemia
MAO inhibitors na salicylates: huongeza athari za insulini
Vitu vingine vyenye mwingiliano na Insulin NPH
Msongo wa mawazo na maambukizi huweza kuongeza mahitaji ya insulini
Maudhi madogo ya Insulin NPH
Maudhi ya mara kwa mara
Maumivu sehemu ya sindano
Uvimbe sehemu ya sindano
Kizunguzungu
Jasho jingi
Njaa ghafla
Maudhi ya mara chache
Lipodystrophy (mabadiliko ya ngozi)
Kuwashwa au vipele
Maumivu kichwa
Maudhi ya nadra sana
Hypoglycemia kali
Athari za mzio kali (anaphylaxis)
Kupoteza fahamu kwa sukari chini sana
Je, endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau dozi, chukua haraka unapoikumbuka isipokuwa ni karibu na dozi inayofuata, basi acha dozi uliyosahau na endelea na ratiba yako ya kawaida. Usichome sindano mbili kwa wakati mmoja.
Uhifadhi wa Insulin NPH
Hifadhi kwenye jokofu (2°C – 8°C) kabla ya kufunguliwa
Baada ya kufunguliwa, hifadhi katika joto la kawaida chini ya 30°C kwa hadi siku 28
Epuka mwanga wa moja kwa moja na joto kali
Usigandishe dawa
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Mei 2025, 11:33:49
Rejea za mada hii:-