Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Mei 2020, 17:23:10

Irbesartan
Utangulizi
Irbesartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu uliyoko katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini II risepta antagonistic (ARBs). Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Avapro
Rangi yake huwa ni vyekundu mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza
Irbesartan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
•75mg
•150mg na
•300mg
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na ibersatan hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu
Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu kwa kuzuia kubadilishwa kwa angiotensini II kwenda angiotensini I hivyo kupunguza shinikizo la damu na kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
• Losartan ( Cozaar)
• Azilisartan (Edarbi)
• Candesartan (Atacand)
• Eprosartan (Teveten)
• Telmisartan (Micardis)
• Valsartan (Diovan)
• Olmesartan (Benicar)
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo;
•Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
• Hutumika kupunguza athari za magonjwa ya figo(dayabetiki nephropathi) kwa wagonjwa wenye kisukari
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
• Voxelotor
• Trandolapril
• Siponimod
• Ramipril
• Quinapril
• Perindopril
• Moexipril
• Lofexidine
• Lithium
• Lisinopril
• Ivosidenib
• Idelalisib
• Fosinopril
• Fedratinib
• Erdafitinib
• Enalapril
• Captopril
• Benazepril
• Apalutamide
• Aliskiren
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa jamii ya ARBs
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
• Wagonjwa wenye figo iliyoferi kufanya kazi
• Wagonjwa wenye Ini lililoferi kufanya kazi
• Wagonjwa wwenye moyo ulioferi kufanya kazi
• Wagonjwa wenye riski ya kupata haipakalemia
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C (mimba yenye umri wa miezi mitatu ya kwanza) na D (Mimba yenye umri wa miezi mitatu ya mwisho) ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni.
Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama na hivyo mtoto anaweza kuipata kwa kunyonya maziwa, isitishwe kupewa kwa mama anayenyonyesha
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
• Haipakalemia
• Kizunguzungu
• Mwili kuchoka
• Kuharisha
• Othostatik haipotesheni
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:31:50
Rejea za mada hii:-