top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Mei 2020 22:30:01

Lansoprazole

Lansoprazole

Lansoprazole ni dawa iliyopo kwenye kundi la proton pump inhibitors yenye uwezo wa kuzuia tindikali kutengenezwa tumboni na hivyo kuwa na uwezo wa kutumika kutibu hali mbalimbali zinanazo sababishwa na uzalishaji wa tindikali tumboni kama ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kucheua tindikali.


Majina mengine ya Lansoprazole


• Prevacid


Fomula ya kikemikali


• C16H13F3N3NaO2S


Jina la kisayansi (IUPAC)la Lansoprazole


• sodium;2-[[3-methyl-4-(2,2,2-trifluoroethoxy)pyridin-2-yl]methylsulfinyl]benzimidazol-1-ide


Fomu na dozi ya Lansoprazole


Dozi ya vidonge vya


• Miligramu 15

• Miligramu 30


Dozi ya tembe za


• 15mg

• 30mg


Dozi ya kimiminika;


• Miligramu 3/mililita


Kazi ya dawa Lansoprazole


• Kutibu vidonda vya tumbo.

• Vidonda vya tumbo vinavyo sababishwa na dawa zilizopo kwenye kundi la NSAID.

• Huchanganywa na dawa nyingine kutokomeza bakteria Helicobacter pylori wanaochangia vidonda vya tumbo.

• Kutibu sindromu ya Zollinger-Ellison

• Hutumika kabla ya kutoa dawa ya usingizi ili kupunguza kuzalishwa kwa tindikali tumboni.

• Kutibu kucheua tindikali

• Kutibu michubuko kwenye koo la chakula kutokana na tindikali.


Namna ya kutumia Lansoprazole


• Tumia kama ulivyo elekezwa na daktari wako.

• Dozi yake hutegemea ugonjwa au hali inayotibiwa.

• Kwa dawa iliyopo kwenye hali ya kimiminika tikisa vizuri kabla ya kutumia.

• Soma maelekezo vizuri kabla ya kutumia.

• Ni vizuri kumeza dakika 30 kabla ya kula.


Namna Lansoprazole Inavyofanya kazi mwilini


Huzuia hatua za mwisho za utoaji wa tindikali tumboni. Hili ni muhimu katika kutibu vidonda vya tumbo,kiungulia na hali zingine zinazo sababishwa tindikali ya tumboni.


Mwili unachofanya kwa dawa ya Lansoprazole


Hufyonzwa na mwiliini kwenda kwenye damu kwa asilimia 81-91, ila kiwango hiki hupungua hadi kwa asilimia 50 -70 ikiwa ikitumika dakika 30 baada ya kula.


Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondolewa sumu


Takamwili za mabaki yake hutolewa kwa njia ya kinyesi (asilimia 67) na mkojo(asilimia 33)


Maudhi madogo madogo ya Lansoprazole


 • Maumivu ya kichwa

 • Kuaharisha

 • Kichefuchefu

 • Maumivu ya tumbo

 • Kutapika

 • Kujamba

 • Kizunguzungu

 • Maumivu ya viungo

 • Homa kwa watoto.

 • Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji kwa watoto.


Kwa kina nani Lansoprazole ni Marufuku kutumika


 • Wagonjwa wenye aleji na lansoprazole

 • Mgonjwa anaetumia dawa zenye rilpivirine


Tahadhari wakati wa kutumia lansoprazole


 • Kuhara wakati wakutumia dawa ya lansoprazole kunaweza kusababishwa na bakteria clostridium difficile.

 • Kutumia dawa hii kila siku zaidi ya mara moja kwa muda mrefu kunaongeza uwezekano wa mifupa kuvunjika kwa urahisi.

 • Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu kama zaidi ya miaka mitatu yaweza kusbabisha upungufu wa vitamini B-12 kwa kupunguza ufyonzwaji wa vitamini hizo.

 • Matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha kiwango cha magnesium kwenye damu kushuka chini ya kiwango cha kawaida.

 • Matumizi ya zaidi ya mwaka yanaongeza atari ya polipsi kwenye tezi zilizo kwenye fandazi.

 • Inaweza leta ugonjwa wa kusambaa wa lupazi erithromatosasi


Muingiliano wa Lansoprazole na dawa nyingine


Lansoprazole isitumiwe pamoja na dawa ya kupunguza makali ya VVU iitwayo Atazanavir kwani hupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha atazanavir kwenye damu.


 • Lansoprazole hupunguza utendaji kazi wa dawa zifuatazo;

 • Ketoconazole

 • Itraconazole

 • Digoxin

 • Dawa za chumvi zenye madini ya chuma

 • Erlotinib

 • Dasatinib


• Kutumia dawa hii pamoja na Clarithromycin pamoja na dawa nyingine kunaweza kusababisha mathara. Hivyo daktarin lazima afahamu atakavyo itumia na dawa nyingine.


• Kutumia kwa pamoja na dawa ya warfarin inaweza kusababisha kuvuja damu nyingi na kuhatarisha maisha. Inabidi kufuatilia muda wa prothrombini


Matumizi ya Lansoprazole wakati ujauzito


Dawa itumike kwa tahadhari kama faida ya kutumia ni kubwa kuliko madhara; Majaribio kwa wanyama yanaonesha madhara na majaribio kwa binadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama na kwa binadamu hayajafanyika.


Matumizi ya Lansoprazole wakati wa kunyonyesha


Ni vyema kujitahidi kuepuka matumizi ya dawa hii wakati wa kunyonyesha kwani hufika kwenye maziwa ya mama na inaweza kumdhuru mtoto anaye nyonya. Uamuzi wa kuitumia wakati wakati wa kunyonyesha utategemea faida na hasara za kuitumia.


Endapo umesahau dozi ya Lansoprazole ufanyenini?


Endapo umesahau kutumia dozi ya Lansoprazole, tumia mara pale utakapokumbuka, endapo muda wa dozi inayofuata umekaribia sana, subiria muda ufike utumie dozi inayofuata kisha kuendelea kwa muda jinsi ulivyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1311.

2.A Textbook of Clinical Pharmacology and TherapeuticS Fifth ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 251.

3.U.S. Food and Drug Administration: https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2017/020406s083,021428s031lbl.pdf imechukuliwa 03/05/2020.

4.Medscape: https://reference.medscape.com/drug/prevacid-solu-tab-lansoprazole-341991 imechukuliwa 03/05/2020.
bottom of page