Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
19 Aprili 2020, 11:30:50

Linagliptin
Linagliptin ni dawa ya inayotumika katika tiba ya ugonjwa wa kisukari aina ya pili, ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4) na hufahamika kwa jina jingine la Tradjenta.
Dawa hii ni ya kumeza, hutuka baada ya kula chakula au kunywa wakati unakula chakula
Rangi ya dawa
mara nyingi huwa nyeupe, hata hivyo mara nyingi hutegemea rangi iliyopendekezwa na kiwanda.
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Alogliptin ni;
• Saxagliptin
• Sitagliptin
• Linagliptin
• Vildagliptin
Linagliptin haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
• Apalutamide
• Benazepril
• Idelalisib
• Ivosidenib
• Lasmiditan
• Voxelotor
Jinsi inavyofanya kazi ;
Hufanya kazi kwa kuongeza kiasi cha homoni za kimetaboli zinazoitwa inkretin ambazo huthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu kwa kuchochea kuzalishwa zaidi kwa homoni ya Insulin, hasa baada ya kula
Hupunguza kiasi cha sukari kinazalishwa na ini kisha kuingia kwenye damu.
Kazi za Linagliptin
Hutumika kwenye matibabu ya kisukari kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili.
Dawa hii haipaswi kutumika kwa;
• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
• Wagonjwa wa Kisukari aina ya kwanza
• Wagonjwa wa dayabetiki ketoasidosisi
Tahadhari kwa dawa hii
• Endapo itatumika pamoja na Insulin huweza kushusha sukari ikawa ya chini sana
• Hatari ya shida katika moyo, inapaswa kutumika kwa uangalifu
• Husababisha pakriataitizi
• Husababisha maumivu ya jointi za mwili
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha;
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Hakuna athari zozote kwa mtoto wakati wa kunyonyesha
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
• Nasofarinjaitizi
• Kuongezeka kwa kolestro mwilini
• Kukohoa endapo itatumika na Metformin na sulphonylurea
• Kuongeza uzito
• Haipoglaisemia
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, Tumia dawa mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umefika. Kama muda wa dozi ingine umefika ruka dozi hii uliyosahau na endelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Januari 2022, 19:39:20
Rejea za mada hii:-