top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

22 Aprili 2020 14:50:46

Losartan

Losartan

Losartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini II risepta antagonisti (ARBs). Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Cozaar.


Dawa jamii ya ARBs hufanya kazi saw ana dawa za ACEIs, uzuri wa dawa za ARBs ni kuwa hazina maudhi ya kupata kikohozi ambacho husababishwa na dawa jamii ya ACEIs. Mtu anapokuwa na madhara ya dawa jamii ya ACEIs hubadilishiwa na kupewa dawa jamiiya ARBs. Wagonjwa wa shinikizo la damu la juu wanapotumia ARBs wanatakiwa kuchunguzwa kuhusu utendaji kazi wa figo, na kiwango cha madini ya potasiamu kwenye damu na kiwango cha shinikizo la damu.


Muda wa kufanya kazi kwa Losartan


Dawa hii huwa na muda mrefu wa kufantya kazi hivyo hutumika mara moja tu kwa siku.


Fomu na uzito wa dawa


Losartan hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu,


•25mg

•50mg na

•100mg


Namna Losartan inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu


Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Lorsatan hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu

Kuzuia homoni ya angiotensini II kufanya kazi yake ya kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu. Matokeo ya utendaji kazi wa losartani ni kuongezeka kwa kipenyo cha mishipa ya damu na hivyo kushuka kwa shinikizo la damu.


Dawa zilizo kundi moja na Losartan


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;


• Azilsartan (Edarbi)

• Candesartan (Atacand)

• Eprosartan (Teveten)

• Irbesartan (Avapro)

• Telmisartan (Micardis)

• Valsartan (Diovan)

• Olmesartan (Benicar)


Kazi ya dawa losartan


Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:


•Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

•Hutumika kupunguza athari za magonjwa ya figo(dayabetiki nephropathi) kwa wagonjwa wenye kisukari

• Hutumika kwenye matibabu ya sindromu ya marfan

• Hutumika kwenye matibabu kutanuka ukuta wa kushoto wa chemba za ventriko


Dawa mwiko kutumika na Losartan


Losartan haipaswi kutumika kwa pamoja na dawa zifuatazo:


• Voxelotor

• Trandolapril

• Siponimod

• Ramipril

• Quinapril

• Perindopril

• Moexipril

• Lofexidine

• Lithium

• Lisinopril

• Ivosidenib

• Idelalisib

• Fosinopril

• Fedratinib

• Erdafitinib

• Enalapril

• Captopril

• Benazepril

• Apalutamide

• Aliskiren


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Losartan


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa jamii ya ARBs


Tahadhari kwa Matumizi ya Losartan


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye figo iliyoferi

• Wagonjwa wenye hatari ya kupata shinikizo la damu la chini na haipakalemia

• Wagonjwa wenye shida ya Ini


Matumizi ya Losartan kwa mama mjamzito


Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kutokana na madhara yake katika figo ya mtoto. Huweza kusababisha kupungua kwa kazi za figo na kuongeza magonjwa na vifo vya watoto wachanga. Endapo mama alikuwa anatumia dawah ii kabla ya ujauzito, akijulikana tu kuwa anamimba dawah ii inapaswa kusimamishwa mara moja.


Matumizi ya Losartan kwa mama anayenyonyesha


Haijulikani kama dawa hii hupita na kuingia kwenye maziwa ila aishauriwi kutumika kwa wamama wanaonyonyesha.


Maudhi ya dawa Losartan

Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni;


• Kikohozi kikavu

• Shinikizo la chini la damu

• Kuishiwa nguvu

• Kichefuchefu

• Haipakalemia

• Maumivu ya mgongo

• Maumivu ya tumbo

• Maumivu ya kichwa

• Kuharisha

• Maumivu ya kifua

• Anemia

• Mwili kuchoka

• Kizunguzungu


Je endapo utasahau dozi yako ya Losartan ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.


Wapi utapata taarifa zaidi kuhusu Lorsartan?


Soma zaidi kuhusu dawa hii na matumizi kwenye ujauzito na kunyonyesha kwenye makala za usalama wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyoneysha sehemu nyingine katika makala za ULYCLINIC

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:41:32

Rejea za mada hii:-

1. Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 213-214

2.Drugs.losartan.https://www.drugs.com/losartan.html. Imechukuliwa 22/4/2020

3.Medscape.losartan.https://reference.medscape.com/drug/cozaar-losartan-342323#3. Imechukuliwa 22/4/2020

4.WebMd.losartan.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6616/losartan-oral/details. Imechukuliwa 22/4/2020

5.MedicinePlus.losartan.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a695008.html. Imechukuliwa 22/4/2020
bottom of page