top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

24 Aprili 2020 05:28:08

Lurasidone

Lurasidone

Utangulizi


Lurasidone ni dawa ya kutibu magonjwa ya akili na hali ya moyo wa mtu mfano magonjwa ya skizofrenia, dipresheni inayoambata na madhaifu ki baipola. Dawa hii ni kizazi kipya kwenye kundi la dawa liitwalo atipiko antisaikotiki.


Atypical antipsychotic ni dawa ambazo husababisha uwepo wa maudhi madogo madogo dalili za parkinsonizimu, simanzi, akathisia, kichefuchefu na agitesheni kwa asilimia 5 ya wagonjwa wanaotumia dawa hii.


Dawa hii inapatikana mfumo wa kidonge milligramu 40 na 80 ambacho hutumika mara moja kwa siku na inapaswa kutumiwa pamoja na chakula angalau kilo kalori 350. Dozi ya dawa inategemea aina ya mgonjwa

Mara baada ya kunywa dawa inachukua muda wa wiki kadhaa(wiki 6 kwa mgonjwa wa skizofrenia) kabla ya dalili kuanza kupotea, unashauriwa kuendelea kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako.


Ufyonzwaji wa dawa tumboni


Dawa hii mara unapoinywa hufyonzwa kwenye utumbo kwa asilimia 9 hadi 19 ya dawa. Ndani ya saa 1-3 dawa hufikia kilele chake kwenye damu.


Uchakatuaji wa dawa mwilini


Umetaboli inafanyika kwenye Ini na mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 80 na asilimia 9 kwa njia ya mkojoDawa hii hutibu


• Kuchanganyikiwa kiakili ama kutawanyika katika kufikiria (skizofrenia)

• Kupunguza msongo wa mawazo (dipresheni)

• Kutibu maradhi ya hisia mseto / ugonjwa wa kubadilika badilika kihisia ( madhaifu ya ki baipola)

• Kupunguza hali ya wasiwasi

• Kupunguza weweseko na halusinesheni


Maudhi madogo madogo ya dawa hii


• Kichefuchefu na kutapika

• Maumivu ya tumbo

• Kuharisha

• Kupata mawazo ya kujiua

• Kukosa usingizi

• Wasiwasi

• Ongezeko la uzito wa mwili

• Kizunguzungu

• Kusinzia

• Kutetemeka kwa mwili

• Uchovu wa mwili

• Haipaprolaktinemia

• Othostatiki haipotensheni

• Lyukopenia

• Nyutropenia

• Agranyulosaitosisi


Angalizo


Tumia dawa hii kwa Umakini kwa watu wafuatao

• Wenye mzio na dawa hii ama aleji nyingine

• Wenye shida ya Ini

• Wenye matatizo ya Figo

• Wenye ugonjwa wa kisukari

• Wenye kifafa

• Wazee wenywe saikosisi kutokana na daimenshia

• Wenye ugonjwa wa Alzheimer's

• Usitumie dawa kisha kuendesha mitambo yam ashine au kuendesha gari

• Usitumie dawa pamoja na pombe kuepuka madhara makubwa yanayoweza kutokea


Usitumie dawa hii pamoja na dawa zifuatazo;


• Usitumie dawa hii pamoja na dawa za fangasi mfano ketoconazole, itraconazole

• Usitumie dawa hii pamoja na baadhi ya antibiotiki mfano clarithromycin, rifampicin

• Usitumie dawa hii pamoja na dawa jamii ya antidepressants mfano fluoxetine


Kundi la dawa wakati wa ujauzito


Dawa hii ipo kundi D la usalama wa dawa kipindi ch aujauzitoKwa Wajawazito


Dawa hii ina madhara kwa wajawazito pale itumiwapo katika kipindi cha mwisho wa Umri wa mimba Inapelekea athari kwa mtoto baada ya kuzaliwa.


Kwa Wanaonyonyesha


Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyeshwa.


Ukisahau dose Nini kifanyike


Kama umesahau kunywa dose yako, kunywa Mara tu unapokumbuka isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, ruka dozi uliyosaau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:29:25

Rejea za mada hii:-

1.FDA.Lurasidone.https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2010/200603s001lbl.pdf. Imechukuliwa 22.04.2020

2.Lurasidone Uses, side effects, interactions at https://www.drugs.com/mtm/lurasidone.html. Imechukuliwa 22.4.2020

3.Lurasidone Uses, side effects, Warnings at https://www.drugs.com/mtm/lurasidone.html. Imechukuliwa 22.4.2020

4.About Lurasidone at https://www.psycom.net/latuda-lurasidone/. Imechukuliwa 22.4.2020

5.Lurasidone Uses, side effects,dosage, Interactions at https://www.rxlist.com/latuda-drug.htm. Imechukuliwa 22.4.2020

6. Lurasidone. https://psychopharmacologyinstitute.com/publication/lurasidone-pharmacokinetics-2145. Imechukuliwa 22.04.2020

7. NCBI.Lurasidone. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3171824/. Imechukuliwa 22.04.2020
bottom of page