top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Juni 2020 05:35:02

Mecamylamine

Mecamylamine

Mecamylamine


Mecamylamine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Inversine hupatikana kama kidonge cha miligramu 2.5 na inaweza kutumika pamoja au pasipo chakula mara mbili au tatu kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na Daktari.


Namna dawa inavyofanya kazi;


Dawa hii ipo kwenye kundi la ganglionic bloka ambalo huzuia homoni ya acetylcholine kuchochea risepta za postsynaptic. Homoni hii hutoka kwenye neva za presynaptic. Homoni ya acetylcholine huwa kama dalaja kati ya risepta hizi mbili, inapozuia basi husababisha taarifa muhimu kuhusu kusinyaza kipenyo cha mishipa ya damu huwa hazisafiri na hivyo hupelekea mishipa ya damu itanuke na kuruhusu damu ipite kirahisi kwa shinikizo dogo


Kazi ya dawa


Dawa hii inatumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu.


Dawa zilizopo kwenye kundi moja na dawa hii ni :


• Trimetaphan.

• Tubocurarine.

• Pempidine.

• Benzohexonium.

• Chlorisondamine.

• Pentamine.


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kutibu shinikizo la juu la damu (Ganglionic Bloka)


• Dawa hii ina matokeo madogo katika kutanua mishipa ya damu kwenye moyo ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili


Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;


• Agrimony

• Bethanechol

• Brimonidine

• Cornsilk

• Forskolin

• Maitake

• Niacin

• Octacosanol

• Reishi

• Tizanidine

• Treprostinil

• Vasopressin


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii.

• Ambao wanatumia Antibayotiki


Dawa inapaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


Dawa hii huweza kupelekea mrija wa urethra kuziba na kuvimba kwa tezi dume


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Kwa mama mjamzito


Inaweza kutumika kwa tahadhari endapo faida zitakuwa ni kubwa kuliko hatari kwa mtoto sababu dawa hii hupita kwenda kondo kwenda kwa mtoto


Kwa mama anayenyonyesha


Inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha sababu huingia kwenye mazima.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Kizunguzungu

• Kuchoka

• Choo kigumu

• Mdomo kuwa mkavu

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Kuzimia

• Kutetemeka


Mengine yanayofanyika Mwilini


Nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 24, dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo kwa asilimia 100


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.RXlist.Mecamylamine.https://www.rxlist.com/inversine-drug.htm. Imechukuliwa 29/6/2020

2.WebMd.Mecamylamine. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-19480/mecamylamine-oral/details .Imechukuliwa 29/6/2020

3.MedScape.Mecamylamine.https://reference.medscape.com/drug/Mecamylamine-342386.Imechukuliwa 29/6/2020

4.Drugbank.Mecamylamine. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00657 .Imechukuliwa 29/6/2020
bottom of page