top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Aprili 2020 11:14:05

Nicardipine

Nicardipine

Utangulizi


Nicardipine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa kalisiamu chaneli bloka. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Cardene IV na Cardene SR hupatikana katika mfumo wa tembe na unga. Rangi ya kidonge mara nyingi ni ya njano na blue iliyopauka kwa mwonekano wa nje wa tembe lakini huweza kubadilika kutokana na aina ya kiwanda kinachotengeneza dawa.


Dawa hii inapaswa kutumika pamoja na chakula au pasipo chakula mara tatu kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari.


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa ili kupata matokeo mazuri kwa wakati.


Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa hii shinikizo la damu litashuka na kuwa kawaida.


Nicardipine hupatikana katika mfumo wa tembe yenye uzito wa Milligram;


• 20 mg

• 30 mg


Namna Dawa inavyofanya kazi;


Ufanyaji kazi wa misuli hutegemea uwepo wa madini ya kalisiamu. Kuingia kwa Kalisimu ndani ya chembe za misuli husaidia misuli kujongea, misuli ya mishipa ya damu inapojongea, huleta shinikizo la damu ndani ya mishipa. Moyo pia unahitaji madini haya ili uweze kufanya kazi ya kusukuma damu mwilini. Dawa za kalisiamu chaneli bloka huzuia kuingia kwa madini haya kwenye chembe za misuli hivyo kuizuai isijongee na matokeo yake ni kuongeza kipenyo cha mishipa ya damu na kupunguza shinikizo la ndani ya mishipa ya damu


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja ni;


• Felodipine

• Isradipine

• Lecarnidipine

• Nifedipine

• Levamlodipine

• Nimonidipine

• Nisoldipine

• Nitrendipine


Kazi za dawa hii ni;


•Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu

•Hutumika kutibu ugonjwa wa anjaina


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi ni;


• Dawa hii hufaa zaidi kwenye mishipa ya moyo zaidi ya Nifedipine, Amlodipine na Felodipine

• Dawa hii ipo kwenye kundi la kwanza la kalisimau chaneli bloka ambazo hutibu shinikizo la kawaida a la kati.


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo


• Cobimetinib

• Conivaptan

• Dantrolene

• Dihydroergotamine

• Eliglustat

• Flibanserin

• Ivabradine

• Lomitapide

• Lovastatin

• Lurasidone

• Naloxegol

• Regorafenib

• Venetoclax

• Saquinavir


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;

• Wagonjwa wenye moyo ulioferi

• Wagonjwa wenye matatizo ya figo na ini


Kundi la dawa wakati wa ujauzito


Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida zitakuwa ni nyingi kuliko hatari kwa mtoto.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


• Maumivu ya kichwa

• Shinikizo la chini la damu

• Kuongeza hali mbaya ya anjaina

• Misuli kuishiwa nguvu

• Kichefuchefu

• Kizunguzungu

• Vipele

• Kukojoa mara kwa mara


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:27:20

Rejea za mada hii:-

1.FDA. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2011/019734s017lbl.pdf. Imechukuliwa 21.04.2020

2.MedScape.Nicardipine.https://reference.medscape.com/drug/cardene-iv-nicardipine-342377. Imechukuliwa 21/4/2020

3.MedLinePlus.Nicardipine.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a695032.html. Imechukuliwa 21/4/2020

4. DrugBank.Nicardipine.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00622. Imechukuliwa 21/4/2020

5. Drugs.Nicardipine.https://www.drugs.com/mtm/nicardipine-oral-injection.html. Imechukuliwa 21/4/2020

6. Goodman and Gilman’s The Pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 ukurasa wa 755
bottom of page