Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Aprili 2020 07:36:09
Nimodipine
Nimodipine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na kuvia kwa damu kwenye uwazi wa sabuarakinoidi.
Kundi la dawa Nimodipine
Nimodipine ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa kalisiamu chaneli bloka.
Majina ya kibiashara
Nimodipine hufahamika kwa majina mengine kama;
Nimotop
Nymalize
Nimodipine na chakula
Kunywa dawa hii saa 1 kabla ya kula au masaa 2 baada ya kula kama utakavyoelekezwa na daktari wako
Haupaswi kunywa au kutumia chakula chenye tindikali saa 1 kabla au masaa 2 baada ya kumeza dawa maana huzuia ufyozwaji wa dawa. Epuka utumiaji wa zabibu baada ya kutumia dawa hii
Fomu na uzito wa Nimodipine
Nimodipine hupatikana katika fomu ya unga na tembe. Tembe huwa yenye uzito wa Milligram 30.
Ufanyaji kazi wa Nimodipine
Ufanyaji kazi wa misuli hutegemea uwepo wa madini ya kalisiamu. Kuingia kwa Kalisimu ndani ya chembe za misuli husaidia misuli kujongea, misuli ya mishipa ya damu inapojongea, huleta shinikizo la damu ndani ya mishipa. Moyo pia unahitaji madini haya ili uweze kufanya kazi ya kusukuma damu mwilini. Dawa za kalisiamu chaneli bloka huzuia kuingia kwa madini haya kwenye chembe za misuli hivyo kuizuai isijongee na matokeo yake ni kuongeza kipenyo cha mishipa ya damu na kupunguza shinikizo la ndani ya mishipa ya damu.
Dawa ya nimodipine ina uwezo mkubwa wa kuzuia kujongea kwa mishipa ya damu ndani ya ubongo kuliko mishipa ya damu sehemu nyingine ya mwili, hii ndo maana hutumika kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa wenye hemoreji ya sabuarakinoidi
Dawa kundi moja na Nimodipine
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Felodipine
Isradipine
Nicardipine
Nifedipine
Levamlodipine
Nicardipine
Nisoldipine
Nitrendipine
Nimodipine hutibu nini?
Hutumika kutibu tatizo la damu kuvia kwenye uwasi wa sabarakinoidi
Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
Upekee wa Nimodipine
Nimodipine ni dawa pekee kwenye kundi hili inavyotumika kutibu hemoreji ya sabuarakinoidi
Mwingiliano wa Nimodipine na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo
Aluminum hydroxide
Apalutamide
Calcium carbonate
Cimetidine
Ibuprofen
Idelalisib
Ivosidenib
Lofexidine
Nefazodone
Sodium bicarbonate
Voxelotor
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Nimodipine
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Tahadhari ya Nimodipine
Kwa Wagonjwa walioferi moyo kabisa
Wagonjwa wenye shida ya figo na ini
Huweza kuongeza mapigo ya moyo kwenda kasi
Huweza kupelekea shinikizo la chini la damu
Nimodipine na ujauzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa Mama mjamzito
Nimodipine kipindi cha kunyonyesha
na haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Nimodipine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kushusha shinikizo la damu kuwa chini zaidi
Kuharisha
Maumivu ya kichwa
Vipele
Moyo kushindwa kufanya kazi
Arrhythmia
Upungufu wa damu
Huweza kupelekea kuvuja damu kwenye mfumo wa umeng’enyaji
Kutapika
Je, kama umesahau dozi yako ya Nimodipine ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya nimodipine, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria ufike kasha endelea na dozi kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:27:31
Rejea za mada hii:-