Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Mei 2020 21:12:26
Nitrendipine
Nitrendipine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kundi la kalisiamu chaneli bloka.
Majina ya kibiashara
Nitrendipine huwa na majina mengine ya kibiashara kama;
1 A Pharma
AbZ-Pharma
AbZ-Pharma
acis Arzneimittel
Adeka
Aliud Pharma
Altana
Apogepha Arzneimittel
Aristo Pharma
Balkanpharma-Dupnitsa
Bayer
Bayer Vital
Baylotensin
Bayniroad
Bayotensin 20mg
Bayotensin 5mg/1ml
Bayotensin mite 10mg
Baypresol
Baypress
Berlin-Chemie
Biosintética
Biosintética, Brazil
Bros
Caltren
Cardiazem
Cenipres
Ditrenil
Dosperopin
Ecatelisin
Egis Pharmaceuticals
Elmor
Enanorm [+ Enalapril]
Eneas [+ Enalapril]
Ferrer Farma
Ferrer Internacional
Ferrer,
Heumann
Hexal
Hexal
Hexal
Hiperdipina
Instituto Sanitas
Intendis
Juta
Jutapress
Kern Pharma, Spain
Krka
Krka
Kyorin Rimedio
Laboratorio Chile, Chile
Laboratorios Andromaco
Libbs
Lisba
Lusopress
Medilat
mibe
Mintlab Co., Chile
Mylan dura
Mylan, France
Nelconil
Nian
Nichi-Iko Pharmaceutical
Nidrel
Nifecard
Nilzipin
Nitregamma
Nitren
Nitren-acis
Nitrencord
Nitrendil
Nitrendilat
Nitrendipin - 1 A Pharma
Nitrendipin AbZ
Nitrendipin Actavis
Nitrendipin AL
Nitrendipin Apogepha
Nitrendipin Aristo
Nitrendipin dura
Nitrendipin Heumann
Nitrendipin JENAPHARM
Nitrendipin Sandoz
Nitrendipin STADA
Nitrendipin-CT
Nitrendipine
Nitrendipine
Nitrendipine Mylan
Nitrendipine-Xinhua Pharm
Nitrendipino Andromaco
Nitrendipin-ratiopharm
Nitrendypina Egis
Nitrepin
Nitrepress
Nitresan
Rafarm
Ratiopharm
S.J.A.
Shu Mai Te
Siam Bheasach
Siu Guan
Stada Arzneimittel
STADA, Spain
Sub-Tensin
Takeda Teva Pharma
Tanabe Mitsubishi Pharma
Tensogradal
Tetrafarma
Towa Yakuhin
UCB Pharma
Unipres
Uriach Group
USV
Vipres [+ Enalapril]
Ying Yuan
Zensei Yakuhin
Nitrendipine na chakula
Unaweza kutumia Pamoja au pasipo chakula
Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa shinikizo la damu litashuka na kuwa kawaida.
Fomu na uzito wa Nitrendipine
Nitrendipine hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa Milligram 20
Ufanyaji kazi wa Nitrendipine
Hufanya kazi kwa kuzuia kalisiamu kuingia kwenye misuli na mishipa ya damu. Kalisiamu huwa na kazi ya kufanya misuli isinyae kwa nguvu, inapozuiwa na dawa hii mishipa ya damu hutanuka na kuongezeka kpenyo, matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Dawa kundi moja na Nitrendipine
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Felodipine
Isradipine
Nicardipine
Nifedipine
Levamlodipine
Nimonidipine
Lecardipine
Nisoldipine
Nitrendipine hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya shinikizo la juu la damu.
Upekee wa Nitrendipine
Nitrendipine huchukua muda mrefu mpaka kushusha shinikizo la damu na huweza kukaa kwa muda mrefu mwilini baada ya dozi kusimamishwa ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi lake.
Mwingilino wa Nitrendipine na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo
Aluminum hydroxide
Apalutamide
Calcium carbonate
Carbamazepine
Cimetidine
Efavirenz
Erythromycin base
Esomeprazole
Ibuprofen
Idelalisib
Isoniazid
Ivosidenib
Lofexidine
Nefazodone
Omeprazole
Pantoprazole
Rabeprazole
Rifabutin
Rifampin
Sodium bicarbonate
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Nitrendipine
Nitrendipine haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye aleji na dawa hii.
Tahadhari ya Nitrendipine
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa walioferi moyo
Wagonjwa wenye shida ya figo na ini
Maudhi ya Nitrendipine
Baadhi ya maudhi madogo ya daw ani
Maumivu ya kichwa
Kuvimba miguu na mikono
Kizunguzungu
Kusikia mapigo ya moyo kusiko kwa kawaida
Kupanua mishipa
Kichefuchefu
Farinjaitizi
Sinusaitizi
Vipele
Je, kama umesahau dozi ya Nitrendipine ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Nitrendipine , tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia, ambapo utakakiwa subiria ufike ili uendelee na dozi kama ulivyopangiwa na daktari wkao.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:27:38
Rejea za mada hii:-