Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Mei 2020 18:21:11
Nizatidine
Nizatidine ni dawa ya kuzuia uzalishaji tindikali inayotumika katik amatibabu ya kucheua tindikali na maradhi mengine yanayotokana na uzalishaji wa tindikali.
Majina ya kibiashara
Majina mengine ya Nizatidine ni
Axid
Acinon
Zanizal
Nizax
Calmaxid
Cronizat
Fomula ya kikemikali
Fomu ya kikemia ya Nizatidine ni C12H21N5O2S2
Jina la kisayansi (IUPAC)
Jina la kisayansi la Nizatidine ni (E)-1-N'-[2-[[2-[(dimethylamino)methyl]-1,3-thiazol-4-yl]methylsulfanyl]ethyl]-1-N-methyl-2-nitroethene-1,1-diamine
Nizatidine hutibu nini?
Nizatidine hutumiika kutibu hali zifuatazo ikiwa yenyewe au mchanganyiko na dawa zingine;
Vidonda vya tumbo
Kiungulia
Kucheua tindikali(GERD)
Kutibu michubuko kwenye koo la chakula ilivyo sababishwa na michubuko ya tindikali (kiungulia).
Husaidia kuzuia damu kuvuja kwenye njia ya juu ya mfumo wa chakula
Hutumiwa wakati mgonjwa akipewa dawa ya usingizi kwa dharura ili kuzuia mgonjwa asicheue tindikali kutoka tumboni.
Zollinger-Ellison
Fomu na uzito wa Nizatidine
Nizatidine hupatikana katika;
Kidonge:-
Miligramu 75
Tembe
Miligramu 150
Miligramu 300
Kimiminika
Miligramu 15/mililita
Chakula na Nizatidine
Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja na au bila chakula.
Sigara na Nizatidine
Epuka matumizi ya sigara wakati wa kutumia nizatidine.
Ufanyaji kazi wa Nizatidine
Nizatidine huzuia homoni ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni ili isishiriki katika kazi hiyo.
Ufyonzwaji wa Nizatidine
Nizatidine hufyonzwa na kuingia kwenye damu kwa asilimia 50 kama ikimezwa, na asilimia 90-100 kama ikichomwa kwenye msuli au ndani ya mshipa wa damu.
Muda wa kuanza kazi
Nizatidine huanza kufanya kazi dakika 30 baada ya kumezwa. Ufanisi wake hufika kilele baada ya saa 0.5 -3 baada ya kumezwa na huweza kufanya kazi mwilini hadi kwa saa 10.
Nusu maisha ya dawa
Asilimia 50 ya kiini cha nizatidine hutolewa nje ya mwili kati ya saa 3- 11 baada ya kumezwa.
Nizatidine na chakula
Ufyonzwaji wa nizatidine hauathiriwi na chakula hivyo dawa hii inaweza kumezwa na chakula ama pasipo chakula.
Umetaboli wa Nizatidine
Dawa hii hufanyiwa umetaboli kwenye ini kabla ya kuanza kufanya kazi.
Utoaji Nizatidine mwilini
Asilimia 90 ya dawa hutolewa baada ya masaa 12 kupitia mkojo na chini ya asilimia 6 hutolewa kwa njia ya kinyesi
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Nizatidine
Nizatidine haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye aleji na dawa ya nizatidine.
Tahadhari ya nizatidine
Matumizi ya nizatidine kwa wazee na wenye shida ya figo dawa hii inaweza kusababisha yafuatayo:-
Kuchanganyikiwa
Kuona maruweruwe
Kupata degedge
Mwili kukosa nguvu
Kwa wagonjwa wenye saratani ya tumbo, kupata nafuu wakati anatumia dawa hii haimaanishi kua saratani imetibika.
Nizatidine isiposaidia kutibu kiungulia baada ya majuma 6-8 ni vyema daktari akafikiria juu ya kutumia dawa za kundi la proton pump inhibita kama dawa mbadala pamoja na vipimo zaidi.
Matumizi ya muda mrefu ya nizatidine yanaweza kusababisha upungfu wa vitamini B 12.
Nizatidine itumike kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na ini.Ufuatiliaji wa karibu unahitajika kwa wagonjwa hawa.
Dawa zenye mwingiliano na Nizatidine
Nizatidine hupendelewa zaidi ya cimetidine ikiwa mgonjwa anatumia warfarin au theophllyne kwakua nizatidine haiathiri utendaji kazi wa dawa hizi kama ilivyo cimetidine.
Nizatidine hupunguza ufanisi wa dawa zifuatazo zinazotegemea sana hali ya tindikali tumboni ili kufanya kazi vizuri na kufyonzwa:-
Ketoconazole
Itraconazole
Digoxin
Dawa za chumvi zenye madini ya chuma
Erlotinib
Dasatinib
Dawa zifuatazo hupunguza ufyonzwaji wa nizatidine:-
Sodium bicarbonate
Calcium carbonate
Magnesium dihydroxide
Magnesium carbonate
Magnesium trisilicate
Aluminium hydroxide
Metoclopramide
Uvutaji wa sigara hupunguza kwa kiasi kikubwa ufyonzwaji wa nizatidine hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya sigara.
Nizatidine huongeza kiwango cha nifedipine kwenye damu kwa 30%
Nizatidine huongeza kiwango cha diazepam kwenye damu.
Matumizi wakati wa ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika kama faida ni kubwa kuliko madhara kwa mtoto, hata hivyo inashauriwa kutumia dawa salama zaidi. Soma zaidi kuhusu daw ahii kwenye makala za dawa na ujauzito.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Dawa hii hufika kwenye maziwa ya mama na hivyo ni vyema kuepuka kuitumia wakati wa kunyonyesha na kutumia dawa salama zaidi. Ikibidi kuitumia basi tahathari lazima zichukuliwe.
Maudhi ya Nizatidine
Maudhi madogo madogo ya nizatidine
Maumivu ya kichwa (asilimia 17)
Maumivu ya tumbo
Mwili kuchoka
Kutopata choo
Kuharisha
kizunguzungu
kukosa usingizi
kichefuchefu
Kuwashwa mwili.
upungufu wa damu ( chini ya asilimi 1)
Matatizo ya ini (chini ya asilimia 1)
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-