Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
3 Mei 2020 14:11:12
Perindopril
Perindopril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kundi la angiotensini konventing enzaimu inhibita (ACEIs).
Majina ya kibiashara
Perindopril hufahamika kwa jina la kibiashara kama Aceon
Perindopril na chakula
Dawa hii inashauriwa kutumika lisaa limoja kabla ya kula chakula kama utakavyoshauriwa na Daktari wako. Tumia dawa hii na maji ya kutosha.
Uzito wa Perindopril
Perindopril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligramu zifuatazo;
2mg
4mg
8mg
Namna Perindopril inavyofanya kazi
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na Perindopril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu
Perindopril huongeza kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensini II na uvunjwaji wa Bradykinin. Kuogezeka kwa kipenyo cha mishipa husababisha kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na hivyo kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza moyo kufanya kazi kupita kiasi
Perindopril hupinga kazi za homoni ya angiotensini II kwenye mishipa ya fahamu ya simpathetiki
Perindopril huongeza uwezo wa figo kupoteza madini ya sodiamu na maji kwa njia ya mkojo kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya aldosterone inayochochewa kuzalishwa zaidi na homoni ya angiotensin II. Homoni ya aldosterone kazi yake ni kutunza maji na madini hayo mwilini
Perindopril huzuia kuharibika kwa kuta za moyo na mishipa ya damu kutokana na shinikizo la damu, kuferi kwa moyo na infaksheni ya mayokadia
Dawa kundi moja na Perindopril
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Perindopril;
Benazepril
Enalapril
Fosinopril
Lisinopril
Lisinopril
Captopril
Moexipril
Quinapril
Ramipril
Kazi ya Perindopril
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi
Hutumika kutibu magonjwa ya mishipa ya moyo
Upekee wa Perindopril
Huweza kusaidia zaidi kupunguza dalili za moyo kuferi ukilinganisha na dawa zingine za kwenye kundi hili.
Mwingiliano wa Perindopril na dawa zingine
Perindopril haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kutokana na kuwa na mwingiliano mkali.
Allopurinol
Aspirin
Azilsartan
Candesartan
Celecoxib
Choline magnesium trisalicylate
Dalteparin
Diclofenac
Diflunisal
Eprosartan
Etodolac
Fenoprofen
Flurbiprofen
Ibuprofen
Indomethacin
Irbesartan
Ketoprofen
Ketorolac
Lofexidine
Losartan
Meclofenamate
Mefenamic acid
Meloxicam
Nabumetone
Naproxen
Olmesartan
Oxaprozin
Piroxicam
Potassium phosphates IV
Pregabalin
Salsalate
Sulindac
Telmisartan
Ttolmetin
Valsartan
Wagonjwa wasioapswa kutumia Perindopril
Perindopril haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs
Angalizo
Perindopril inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wasio toa mkojo
Wagonjwa Wenye shida ya figo
Wagonjwa wa haipatrophic kadiomayopathi
Perindopril na ujauzito
Inapaswa kutumika kwenye hali ya hatari tu endapo hakuna dawa nyingine salama ya kutumika kwa mama mjamzito.
Perindopril wakati wa kunyonyesha
Haishauriwi kutumika kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama.
Maudhi ya Perindopril
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Maumivu ya kichwa
Kukohoa
Kizunguzungu
Maumivu ya mgongo
Kuhisi mapigo ya moyo
Kuwa na hali ya huzuni
Matatizo ya hedhi
Matatizo ya kulala
Maumivu ya kifua
Kichefuchefu
Kutapika
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:26:13
Rejea za mada hii:-