Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
19 Aprili 2020 11:15:06
Phenformin
Ni dawa ya kumeza iliyokuwa ukitumika katika matibabu kisukari aina ya pili ila kwa sasa imeondolewa sokoni kutokan ana madhara yake. Phenformin ipo kundi la dawa la Biguanide.
Majina ya kibiashara
Phenformin ilikuwa ikiuzwa kwa majina ya kibiashara kama
Bidiabe [+ Chlorpropamide]
Sanofi-Aventis, Italy
Gliben F [+ Glibenclamide]
Abiogen Pharma, Italy
Glinorboral [+ Glibenclamide]
Silanes, Mexico
Glinorboral Compuesto [+ Glibenclamide]
Silanes, Mexico; Silanes, El Salvador
Kwanini imeondolewa sokoni?
Phenformin imeondolewa sokoni toka mwana 1977 kutokana na madhara yake ya kusabababisha kifo kutokana na laktiki asidosisi. Laktiki asidosis ni hali inayotokea kama uzalishaji wa kemikali laktiki asidi ni mkubwa. Baadhi ya nchi bado zinatumia dawa hii.
Dawa kundi moja na Phenformin
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Metformin ni zifuatazo;
Proguanil
Buformin
Chlorhexidine
Metformin
Chlorproguanil
Cycloguanil
Buformin kama ilivyo Phenformin ilizuiliwa kutumika pia miaka ya 1970.
Phenformin inavyofanya kazi
Hufanya kazi ya kupunguza kiasi cha sukari kinachotolewa na Ini kwenda kwenye damu.
Hupunguza ufyozwaji wa glukosi kwenye utumbo mdogo
Hufanya seli Beta za kongosho kuzalisha homoni ya insulin
Phenformin hutibu nini?
Phenformin ilikuwa ikitumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili ambacho mara nyingi husababishw ana uzalishwaji wa mdogo wa insulin. Lakini kwa sasa haitumiki kutokana na athari zake za kusabababisha Laktiki Asidosisi.
Hutumika kutibu baadhi ya saratani kwa uwezo wake wa kuzuia ukuaji wa seli na ukuaji wa uvimbe kama saratani ya matiti, utumbo mpana na tezi dume.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Phenformin
Dawa hii haipaswi tumika kwa wagonjwa wenye;
Mzio na dawa hii
Moyo ulioferi
Dayabeetiki ketoasidosisi
Maambukizi makali kwenye fogo
Kulewa
Upumuaji wa shida
Angalizo
Tahadhari ya Phenformin
Utumiaji wa pombe na Phenformin huweza kupelekea hali mbaya ya laktiki asidosisi
Husababisha tezi ya adreno kushindwa kufanya kazi vizuri
Husababisha tezi pituitari kushindwa kufanya kazi zaidi
Huweza kuathiri ufyozwaji wa Vitamin B12
Phenformin kwa anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama wajawazito na wamama wanaonyonyesha
Baadhi ya maudhi madogo ya Phenformin
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Kuharisha kidogo
kuchoka
Kuongezeka kwenye damu kiwango cha laktiki asidi
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:26:20
Rejea za mada hii:-