Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Aprili 2020, 06:50:00

Piroxicam
Ni dawa kwa ajili ya kutuliza maumivu makali ya mwili, uvimbe wa jeraha na kukakamaa kwa jointi kutokana na ugonjwa wa athraitizi. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazojulikana kama NSAIDS. Hupatikana mfumo wa vidonge.
Namna Piroxicam inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi yake ya kwa kuzuia uzalishwaji wa prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa husababisha homa Pamoja na uvimbe kwenye sehemu ya mwili yenye tatizo.
Umetaboli wa dawa Piroxicam na utolewaji taka mwilini
Umetaboli wa Dawa hii Ni hufanyika kwenye Ini na Utoaji taka mwili kupitia Figo
Fomu na uzito wa dawa Piroxicam
Inapatikana kma tembe yenye milligramu 10 na 20mg
Matumizi ya Piroxicam na chakula
Inapaswa kutumika pamoja na chakula au maji mengi(maji yenye ujazo sawa na chupa moja ya soda) ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kwenye mfumo wa gastrointestino.
Magonjwa yanayotibiwa na Piroxicam
Kutibu maumivu ya mwili
Kupunguza uvimbe
Kutibu arthraitis, osteoarthraitizi
Maudhi madogo ya Piroxicam
Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya tumbo
Kupata kiungulia
Kuharisha
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Uchovu wa mwili
Angalizo kwa watumiaji wa Piroxicam
Tumia kwa Umakini Dawa hii kwa watu wafuatao
Wenye shida ya Ini
Wenye matatizo ya Moyo
Wenye shida ya Figo
Wenye mzio wa Naproxen au dawa zingine nyingine
Wenye vidonda vya tumbo(tumia pamoja na antiasidi kuzuia madhara)
Wenye pumu (asthma)
Dawa zisizopaswa kutumika na Piroxicam
Dawa hii hairuhusiwi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kutokana na madhara yanayowez akujitokeza;
Lisinopril
Methotrexate
Methyl aminolevulinate
Moexipril
Pemetrexed
Perindopril
Quinapril
Ramipril
Aminolevulinic ya kumeza
Aminolevulinic ya kupaka
Apixaban
Benazepril
Captopril
Enalapril
Erdafitinib
Fosinopril
Ketorolac
Siponimod
Tacrolimus
Trandolapril
Matumizi ya Piroxicam wakati wa ujauzito
Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi ya mwanzoni na miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.
Matumizi ya Piroxicam kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha, dawa hii hupita katika na kuingia kwenye maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Ukisahau kutumia dose ya Piroxicam ufanyenini?
Kama umesaau kutumia dose yako unaweza tumia Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, acha dozi uliyoruka na kunywa dozi ingine kwa mud auliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Agosti 2023, 19:42:12
Rejea za mada hii:-