Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Aprili 2020 08:52:05
Propranolol
Propranolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la beta bloka.
Majina ya kibiashara
Propranolol kwa jina jingile la Inderal.
Fomu na uzito wa Propranolol
Kidonge chenye uzito wa miligramu,
5mg na
10mg
Tembe chenye uzito wa miligramu,
10mg
20mg
40mg
60mg
80mg
Maji yenye uzito wa miligramu 1 kwa mililita moja 1
Unga wenye ujazo wa
Miligramu 20 kwa mililita 5 (20mg/5ml)
Miligramu 40 kwa mililita 5 (40mg/5ml)
Ufyonzwaji wa Propranolol na nusu maisha yake
Propranolol hufyonzwa vyema kwenye mfumo wa chakula kisha huingia kwenye mzunguko wa damu, kiwango cha juu kabisa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 1-4 baada ya kunywa dozi ya kidonge. Mara baada ya kunywa dawa bila chakula kiwango sawia kwenye damu ambacho hakibadiliki hufikiwa ndani ya masaa 12-14 ikitumiwa bila chakula na 11.5- 15.5 ikitumika pamoja na chakula chenye mafuta.
Propranolol na chakula
Tumia dawa hii pamoja na vyakula vyenye protini ili kuongeza ufyonzaji wake. Tafiti zinaonyesha ufyonzwaji huongezeka kwa asilimia 50 endapo itatumia Pamoja na vyakula vyenye protini.
Umetaboli wa Propranolol
Propranolol hufanyiwa umetaboli kwenye ini na asilimia 25 tu ya dawa mama huweza kupita kama ilivyo kwenda kwenye mzunguko wa damu mara baada ya kupita kwenye ini.
Utoaji dawa Propranolol mwilini
Propranolol hutolewa mwilini kwa njia kuu ya mkojo.
Namna Propranolol inavyofanya kazi
Dawa ya Propranolol pamoja na kuwa kundi la dawa la Beta bloka, ufanyaji kazi wake wa kushusha shinikizo la juu la damu bado haufahamiki. Hata hivyo vitu vinavyochangia dawa hii kushusha shinikizo la damu la juu ni;
Kupunguza mzigo wa moyo kufanya kazi
Kuzuia figo kuzalisha homoni renini
Kupunguza mfumo toniki wa simpathetiki kwenye kituo cha vasomota kilicho ndani ya ubongo
Dawa zilizo kundi moja na Propranolol
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Acebutolol (Sectral)
Betaxolol (Kerlone)
Bisoprolol (Zebeta, Ziac)
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor)
Nebivolol (Bystolic)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Propranolol hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya anjaina
Hutumika kwenye matibabu ya kutetemeka mwili kutokana na hofu (trema)
Hutumika kwenye matibabu ya feochromosaitoma
Hutumika kwenye matibabu ya shinikizo la juu la damu kwenye Ini
Mwingiliano wa Propranolol na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kwa kuwa huwa na mwingiliano mkali;
Verapamil
Timolol
Sotalol
Saquinavir
Rivastigmine
Penbutolol
Nebivolol
Nadolol
Metoprolol
Lofexidine
Labetalol
Esmolol
Diltiazem
Digoxin
Clonidine
Celiprolol
Carvedilol
Bisoprolol
Betaxolol
Acebutolol
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Propranolol
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa zingine jamii Beta bloka
Wagonjwa wenye asthma
Wagonjwa wenye moyo kuferi
Angalizo
Propranolol hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye asthma
Wagonjwa wenye Magonjwa ya kifua
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Propranolol na ujauzito
Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo amna dawa nyingine ya mbadala ya kummpa mama mjamzito.
Propranolol kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa maziwa ya mama anayenyonyesha yanaweza kuwa na kiasi gani cha dawah ii kwenye maziwa ya mama hivyo itumike kwa uangalifu.
Maudhi ya Propranolol
Baadhi ya maudhi madogo ya Propranolol ni;
Haipotesheni
Anthropathi
Haipoglaisemia
Kuwa na uchovu
Ukosefu wa usingizi
Kichefuchefu
Haipalipidemia
Haipakalemia
Kupata shida ya kupumua
Je kama umesahau dozi ya Propranolol ufanyaje?
Kama umesahau dozi yako ya Propranolol, tumia mara pale utakapokumbuka, isipokuwa kama muda wa kunywa dozi inayofuata imekaribia sana ambapo utatakiwa kunywa dozi inayofuata tu kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:24:57
Rejea za mada hii:-