Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Aprili 2020, 05:28:31

Quinapril
Quinapril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs.
Jina la kibiashara
Quinapril huwa maarufu pia kwa jina la kibiashara la Accupril.
Fomu na uzito wa Quinapril
Dawa hii hupatikana kaa kidonge chenye uzito wa miligramu;
5mg
10mg
20mg na
40mg
Namna Quinapril inavyofanya kazi
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na periondopril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu
Hutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.
Dawa zilizo kundi moja na Quinapril
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Benazepril
Captopril
Enalaprili
Fosinopril
Lisinopril
Moexipril
Perindopril
Quinapril hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi
Hutumika kwa kupunguza athari za magonjwa ya figo (dayabetiki neohropathi) kwa wagonjwa wenye kisukari
Dawa zenye wingiliano na Quinapril
Quinapril haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kutokana na kuwa na mwingiliano mkali;
Valsartan
Tolmetin
Telmisartan
Sulindac
Salsalate
Sacubitril/valsartan
Sacubitril/valsartan
Pregabalin
Piroxicam
Oxaprozin
Olmesartan
Naproxen
Nabumetone
Meloxicam
Mefenamic acid
Meclofenamate
Losartan
Lofexidine
Ketorolac
ketoprofen
Irbesartan
Indomethacin
Ibuprofen
Flurbiprofen
Fenoprofen
Etodolac
Eprosartan
Diflunisal
Diclofenac
Celecoxib
Candesartan
Azilsartan
Aspirin
Aliskiren
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Quinapril
Quinapril haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs
Angalizo
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye shinikizo la chini la damu
Quinapril kwa mama mjamzito
Quinapril haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni, endapo mama alikuw aanatumia dawa hii, anapofahamika kuwa ana ujauzito inatakiwakusimamishwa mara moja.
Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.
Quinapril kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa Quinapril kuingia kwenye maziwa ya mtoto hivyo dawa itumike kwa tahadhari
Maudhi ya Quinapril
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Maumivu ya kichwa
Kukohoa
Kizunguzungu
Maumivu ya Mgongo
Kichefuchefu
Kuharisha
Shikizo la chini la damu
Mwili kuchoka
Kutapika
Kuwa na vipele kwenye Ngozi
Je kama umesahau dozi ya Quinapril ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria ufike ndipo unywe dozi moja na kuendelea kama ulivyoshauriw ana daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:25:03
Rejea za mada hii:-