top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

3 Mei 2020 07:32:21

Remdesivir

Remdesivir

Remdesivir ni dawa jamii ya antivairo yenye uwanja mpana katika matibabu ya virusi mbalimbali vya RNA. Kwa mara ya kwanza dawa hii iliruhusiwa na shirika la dawa la marekani (FDA) kutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa virusi vya ebola na Marburg. Licha ya dawa hii kushindwa kutibu magonjwa hayo, kwa sasa shirika la dawa duniani na kampuni ya Gilead sciences linafanya uchunguzi wa dawa hii dhidi ya matibabu ya virusi vya corona au ugonjwa wa COVID-19.


Remdesivir hutibu nini?


Dawa hii imekuwa ikitumika kwenye matibabu ya ebola toka mwaka 2013 huko mangharibi ya Afrika. Mwaka 2019 maafisa afya wa Kongo walitangaza kuwa dawa hii ina ufanisi kidogo sana ukilinganisha na dawa za mAb114 na REGN-EB3 hivyo ilisimamishwa kutumika.


January 2020 dawa hii imefanyiwa uchunguzi na shirika la dawa marekani (FDA) pamoja na kampuni ya Gilead sciences iliyogunduwa dawa hii na ikaonyesha kuwa inauwezo wa kupunguza dalili kwa wagonjwa wa COVID 19. Remdesivir imeonekana kuleta matumaini ya baadae kwenye tiba ya ugonjwa huu. Wagonjwa waliotumia dawa hii wameonekana kupata unafuu haraka Zaidi kuliko wale ambao hawajatumia. Dawa hii imekuwa moja ya dawa nne


Ufanyaji kazi wa Remdesivir


Dawa hii hufanya kazi ya kuzuia kuzaliana kwa kirusi mwilini kwa kupinga uzalishaji wa RNA ya kirusi


Mwingilino wa Remdesivir na dawa zingine


Chakula na dawa zifuatazo zinapunguza ufanisi wa dawa hii


 • Aspirin

 • Beta-Naphthoflavone

 • Broccoli, alizeti, na nyama

 • Carbamazepine

 • Dawa za mesto-Artemisinin

 • Enzalutamide

 • Insulin

 • Methylcholanthrene

 • Modafinil

 • Nafcillin

 • Norethisterone

 • Omeprazole

 • Phenobarbital

 • Phenytoin

 • Prednisone

 • Primidone

 • Rifampicin

 • St john wort’s

 • Tumbaku


Remdesivir na dawa


Chakula na dawa zinazoongeza ufanisi wa dawa hii ni


 • Juisi ya zabibu

 • Forskolin


Maudhi ya Remdesivir


 • Maudhi makubwa ya dawa hii ni

 • Kuferi kwa mfumo wa upumuaji

 • Manjano

 • Haipoalbuminemia(kushuka kwa kiwango cha protini kwenye damu)

 • Kushuka kwa kiwango cha chembe nyekundu za damu

 • Kushuka kwa chembe sahani za damu(thrombosaitopenia

 • Kuongezeka kwa vimeng’enya vya ini kwenye damu

 • Mzio kwenye eneo sindano ilipochomwa

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:25:32

Rejea za mada hii:-

1.Cytochrome P450 inducers. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/cytochrome-p450-inducer. Imechukuliwa 3.05.2020

2.Efects of food on cytochrome p450. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5424325/. Imechukuliwa 3.05.2020

3.Remdesivir. letter of authoritization. https://www.fda.gov/media/137564/download. Imechukuliwa 3.05.2020

4.USAMRIID. Antiviral Compound Provides Full Protection from Ebola Virus in Nonhuman Primates. https://web.archive.org/web/20161224000431/http://www.usamriid.army.mil/press_releases/Travis%20ID%20Week%20FINAL.pdf. Imechukuliwa 3.05.2020

5.NIH. Remdesivir clinical trial. https://www.niaid.nih.gov/news-events/nih-clinical-trial-shows-remdesivir-accelerates-recovery-advanced-covid-19. Imechukuliwa 03.05.2020
bottom of page