top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Mei 2020, 09:19:03

Reserpine

Reserpine

Reserpine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kundi la Rauwolfia alkaloid. Dawa hii hutokana na mizizi ya mmea unaoitwa Rauwolfia serpentine na vomitoria.


Majina ya kibiashara


Reserpine huwa maarufu kwa jina la Serpasil na hutumika pamoja na dawa zingine katika kushusha shinikizo la juu la damu.



Reserpine na chakula


Reserpine inaweza kutumika pamoja na au bila chakula, tumia kama utakavyoelekezwa na Daktari.


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyoitikia dawa.


Fomu na uzito wa Reserpine


Reserpine hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;


  • 0.1 mg

  • 0.25 mg


Namna Reserpine inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwenye mfumo wa fahamu wa kati na pembeni kwa kuzuia utendaji kazi wa homoni zinazoongeza shinikizo la damu ambazo ni norepinephrine, dopamine na serotonin. Kufanya kazi kwa dawa hii hupelekea mapigo ya moyo kwenda kawaida na kupunguza shinikizo la damu.


Reserpine hutibu nini?


Reserpine inatumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu.

Reserpine hutumika kutibu wagonjwa wa matatizo ya akili.


Dawa hii haitumiki sana kutokana na kuwa na mauzi mengi kwenye mfumo wa kati wa neva.


Upekee wa Reserpine kwenye kundi lake


Dawa hii huuzwa bei nafuu ukilinganisha na dawa zingine za kushusha shinikizo la juu la damu na hivyo hutumika sana kwa nchi ambazo ziaendelea.


Mwingiliano wa Reserpine na dawa zingine


Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;


  • Esketamine ya kuweka puani

  • Lemborexant


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Reserpine


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii

  • Wagonjwa wenye vidonda vya tumbo

  • Wagonjwa wenye historia ya hali ya huzuni

  • Wagonjwa wenye historia yam awe kwenye figo


Angalizo


Reserpine inapaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa wenye historia ya haipotension.

  • Wagonjwa wenye historia ya pumu, ugonjwa wa Parkison na shida ya figo.


Reserpine kwa mama mjamzito


Inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida zitakuwa ni kubwa kuliko hatari kwa motto,Tafiti kwa wanyama zinaonyesha yapo madhara kwa motto.

Reserpine kwa mama anayenyonyesha


Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu inatolewa kwenye maziwa.


Maushi ya Reserpine


Baadhi ya maudhi madogo ya Reserpine ni


  • Maumivu ya kifua

  • Mapigo ya moyo kushuka

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kuwa na hali ya huzuni

  • Kuongezeka uzito

  • Kuchoka

  • Kutokuona vizuri


Nusu maisha ya Reserpine


Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 2.5 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa5.


Utoaji Reserpine mwilini


Dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo kwa asilimia 12 na kwa njia ya kinyesi kwa asilimia 60.


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Kama ukisahau kutumia Reserpine tumia mara pale utakapokumbuka na kama muda wa dozi nyingine umekaribia subiria muda ufike kisha unywe katika dozi kama ulivyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023, 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman’s The Pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 Ukurasa wa 418 na 776

2.WebMd.Reserpine.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8703/reserpine-oral/details. Imechukuliwa 28.05.2020

3.MedScape.Reserpine.https://reference.medscape.com/drug/serpasil-reserpine-oral/details. Imechukuliwa 28.05.2020

4.Drugbank.Reserpine.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00206.Imechukuliwa 28.05.2020

5.MedLinePlus.Reserpine.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a601107.html.Imechukuliwa 28.05.2020

6. PUBCHEM. https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Reserpine. Imechukuliwa 28.05.2020
bottom of page