Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Mei 2020, 09:26:03

Risperidone
Risperidone ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya magonjwa ya akili.
Majina ya kibiashara ya Risperidone
Risperidone huuzwa katika jina la risperidal
Fomu
Risperidone hupatikana katika mfumo wa kidonge na kimiminika kutumia kwa kuchomwa sindano.
Dawa kundi moja na Risperidone
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Quetiapine
Olanzipine
Aripiprazole
Ziprasidone
Jinsi Risperidone inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kufunga kwa muda milango(risepta) ya dopamine na serotonin inayotumiwa na homoni hizo. Homoni za dopamine na serotonin hufanya kazi kama nyurotransmita kudhibiti hali ya mawazo, hisia na tabia za mtu. Milango ya homoni hizi inapofungwa huzuia utendaji kazi wa homoni na kupotea kwa dalili za ugonjwa.
Risperidone hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa wa skizofrenia
Hutumika kwenye matibabu ya baipola mania
Hutumika kweney matibabu ya ugonjwa wa Postitraumatiki stress disoda
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye mijongeo isiyo ya kawaida kama mfano macho, miguu na mikono
Dawa zenye mwigiliano na Risperidone
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amiodarone
Apomorphine
Benzhydrocodone
Bromocriptine
Cabergoline
Dacomitinib
Disopyramide
Dopamine
Entrectinib
Erdafitinib
Fluoxetine
Glasdegib
Hydrocodone
Hydroxychloroquine sulfate
Ibutilide
Indapamide
Ivosidenib
Lasmiditan
Levodopa
Lisuride
Macimorelin
Mefloquine
Methyldopa
Ondansetron
Pentamidine
Pimozide
Pitolisant
Pramipexole
Procainamide
Propafenone
Quinidine
Ropinirole
Safinamide
Sodium oxybate
Sotalol
Vandetanib
Vemurafenib
Vilanterol
Angalizo
Tahadhari ya Risperidone
Huweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha chembechembe nyeupe za damu
Haipaswi kutumika kwa tahadhari kwa mgonjwa wa Parkinson na Dementia
Huweza kupelekea Kiharusi
Huweza kuathiri uwezo wa mtu kusimama kwa muda mrefu
Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye aleji na dawa hii
Matumizi ya Risperidone kwa mama mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Matumizi ya Risperidone kwa mama anayenyonyesha
Kwa mama anayenyonyesha haipaswi kutumika sababu hupita kwenda kwenye maziwa na hivyo kumpata mtoto
Maudhi ya Risperidone
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kulala kupita kiasi
Kuwa na woga na wasiwasi
Kicwa kuuma
Rhinitis
Kuchoka
Parkinsonism
Kuongeza hamu ya kula
Kutapika
Kutokwa na udenda
Kujikojolea
Kutetemeka
Nasopharyngitis
Kutokwa na maji puani
Kujikojolea kitandani wakati wa usiku
Choo kigumu
Kichefuchefu
Tumbo kuuma
Vipele
Mapigo ya moyo kusikika katika hali isiyo ya kawaida
Je endapo dozi yako itasahaulika utafanyaje?
Endapo umesahau kutumia risperidone, tumia mara pale atakapokumbuka. kama muda wa dozi ingine umekaribia sana, subiri ili kuitumia katika muda kama ulivyopangiwa na daktari wako. Kamwe usitumie dozi zaidi ya moja kamahujashauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-