Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Juni 2020 05:44:15
Sodium Nitroprusside
Sodium Nitroprusside ni dawa Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Vasodilator inayotumika kushusha shinikizo la juu la damu.
Majina ya ibiashara
Sodium Nitroprusside dawa ni maarufu kwa jina la Nitropress
Fomu na uzito wa Sodium Nitroprusside
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kimiminika kwa ajili ya sindano katika ujazo ufuatao;
25 Mg/Ml
0.5 Mg/Ml
Ufanyaji kazi wa Sodium Nitroprusside
Dawa jamii ya vasodilator ikiwa pamoja na Sodium Nitroprusside hufanya kazi zifuatazo ili kushusha shinikizo la damu;
Hulegeza misuli kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya ipanuke. Kupanuka kwa mishipa ya damu hupelekea damu kupita kwa taratibu bila shinikizo, nah ii huchangia kushuka kwa shinikizo la damu.
Dawa zilizo kundi moja na Sodium Nitroprusside
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Nitroglycerin
Isosorbide mononitrate
Isosorbide dinitrate
Hydralazine
Minoxidil
Fenoldopam
Sodium Nitroprusside Hutibu nini?
Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu
Hutumika kuthibiti Haipotension wakati wa upasuaji
Hutumika kwa mgonjwa mwenye moyo ulioferi kwa kuthibiti shinikizo la juu damu kwenye chumba cha kushoto cha Ventrical
Upekee wa Sodium Nitroprusside
Dawa hii huweza kutanua mishipa ya ateri tofauti na dawa zingine ambazo hutanua Vena hivyo ni imara zaidi katika kushusha shinikizo la juu zaidi la damu
Meingiliano wa Sodium Nitroprusside na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amlodipine
Benazepril
Bretylium
Clevidipine
Clonidine
Dapsone topical
Dichlorphenamide
Diltiazem
Felodipine
Guanfacine
Isradipine
Maraviroc
Nicardipine
Nifedipine
Nisoldipine
Sildenafil
Tadalafil
Tetracaine
Vardenafil
Verapamil
Wagonjwa wasioapswa kutumia Sodium Nitroprusside
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Vasodilator
Angalizo
Sodium Nitroprusside inaweza kupeleke
Haiponatremia
Haipothyroidism
Ini au figo kushindwa kufanya kazi
Matumizi ya Sodium Nitroprusside kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Matumizi ya Sodium Nitroprusside kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama hutolewa kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Maudhi ya Sodium Nitroprusside
Baadhi ya maudhi madogo ya Sodium Nitroprusside ni;
Haipotension
Maumivu ya kichwa
Kutokwa na jasho
Kizunguzungu
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Oliguria
Kuwashwa sehemu ya sindano
Kutokwa vipele
Nusu maisha na utoaji dawa Sodium Nitroprusside
Nusu maisha ya dawa mwilini ni dakika 2 na Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo
Kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia Sodium Nitroprusside, tumia mara pale utakapokumbuka. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana subiria muda ufike ili uendelee na dozi hiyo kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-