top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

28 Machi 2020 13:44:01

Sulfamethoxazole na Trimethopin

Sulfamethoxazole na Trimethopin

Sulfamethoxazole na Trimethopin ni dawa ya antibayotiki ambayo imepewa ufupisho wa Co – Trimoxazole inayotumika katika matibabu ya maradhimbalimbali yanayosababishwa na bakteria.


Bakteria wanaodhuriwa na Co – Trimoxazole


Baadhi ya bakteria ambao hutibiwa na dawa hii ni bakteria jamii ya:


 • Staphylococcus aureus

 • Staphylococcus epidermidis

 • Staphylococcus pyogenes

 • Streptococci kundi la Viridans

 • Escherichia coli

 • Proteus mirabilis

 • Proteus morganii

 • Proteus rettgeri

 • Salmonella typhi

 • Klebsiella species

 • Brucella abortus

 • Yersinia enterocolitica


Co – Trimoxazole hutibu nini?


Dawa ya jamii ya Sulfamethoxazole na Trimetropin hutumika kutibu magonjwa yafuatayo:


 • UTI

 • Bronkaitizi

 • Shigellosisi (Ugonjwa wa kuhara ambao huambatana na tumbo kuuma)

 • Kuhara kwa muda mfupi -kunaosababishwa na bakteria wa Escherichia Coli

 • Nimonia ya Pneumosisti jirovesii: Nimonia ambayo hutokea sana kwa wagonjwa wa VVU na UKIMWI

 • Homa ya mapafu ya kuambukizwa kwenye jamii

 • Maisetoma

 • Otaitizi media


Maudhi ya Co – Trimoxazole


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na:


 • Kukosa hamu ya kula

 • Kichefuchefu

 • Kutapika

 • Kutokwa na Vipele

 • Anemia ya Aplastiki

 • Kupata mzio

 • Kuwashwa ngozi

 • Haipakalemia

 • Upungufu wa Foleti mwilini


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Co – Trimoxazole


Dawa hii haitumiki kwa watu wafuatao :


 • Watoto chini ya miezi miwili

 • Mama mjamzito anayekaribia kujifungua (Term pregnancy)

 • Kwa mtu mwenye anemia ya meganoblastic

 • Watu wenye matatizo ya ini

 • Watu wenye matatizo ya figo


Matumizi ya Co – Trimoxazole kwa mama mjamzito


Kwa maelezo kuhusu mama mjamzito ingia kwenye sehemu ya ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha ndani ya tovuti hii.


 • Matumizi ya Co – Trimoxazole wakati wa kunyonyesha

 • Kwa maelezo kuhusu mama mjamzito ingia kwenye sehemu ya ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha ndani ya tovuti hii.


Kama umesahau dozi ya Co – Trimoxazole ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi yako ya Co – Trimoxazole , tumia pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia saba achana na dozi uliyosahau kisha subiria muda ufike na endelea na dozi kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:22:37

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman's,The pharmacology Basis of therapeutic ,Ukurasa wa 1465-1465

2.A text book of Clinical pharmacology and therapeutic kilichoandikwa na Jama M Ritter Ukurasa wa 330

3.Modern pharmacology with Clinical application kilichoandikwa na Charles R. Craig ukurasa wa 516-520

4. BNF 76 September 2018 – March 2019 kurasa wa 552
bottom of page