Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Aprili 2020 09:00:45
Taspoglutide
Taspoglutide ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti.
Majina ya kibiashara
Taspoglutide huwa maarufu kwa majina mengine ya kibiashara kama ipsen na roches.
Namna Taspoglutide inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuchochea kongosho kuzalisha homoni ya Insulin mara kiwango cha sukari kinapoongezeka kwenye damu.
Homoni ya Insulini husaidia seli za mwili kutumia na kuhifadhi sukari na hivyo kuiondoa kwenye dmau. Kufanya hivi kiwango cha sukari hupungua sana kwenye damu.
Dawa kundi moja na Taspoglutide
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja ni;
Exenatide
Lixisenatide
Semaglutide
Dulaglutide
Liraglutide
Taspoglutide hutibu nini?
Hutumika kudhibiti kiasi cha sukari kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili
Upekee wa Taspoglutide na dawa kundi GlP1 Agonisti
Sindano ya dawa hii huweza kuthibiti kiasi cha sukari mara mbili zaidi ya dawa zingine kwenye kundi hili
Dawa hii huleta maudhi mengi yasiyoelezeka katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu na kutapika pamoja na mzio kwa watumiaji wengi
Mwingiliano wa Taspoglutide na dawa zingine
Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;
Acarbose
Aripiprazole
Asenapine
Atorvastatin
Cortisone
Darunavir
Desogestrel
Dexamethasone
Drospirenone
Enalapril
Eprosartan
Estradiol
Estropipate
Ethinylestradiol
Etonogestrel
Fludrocortisone
Fuphenazine
Fosamprenavir
Fosinopril
Glimepiridine
Glipizide
Glyburide
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Taspoglutide
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hiyo
Mwenye shida ya figo
Angalizo
Tahadhari ya Taspoglutide;
Sio mbadala wa Insulin
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya kwanza
Huweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi
Matumizi ya Taspoglutide kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha
Maudhi ya Taspoglutide
Baadhi ya maudhi madogo ya taspoglutide
Kichefuchefu
Kuhara
Kutapika
Choo kuwa kigumu
Kuvimba sehemu iliyochomwa sindano
Maumivu ya kichwa
Kupunguza hamu ya kula
Kuchoka
Kizunguzungu
Maumivu ya tumbo
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi ya Taspoglutide, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana usinywe mpaka muda utakapofika kasha endelea kwa muda uliopangiwa na daktari wako. Usinywe dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:22:44
Rejea za mada hii:-