Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020, 10:41:43
Tenofovir
Tenofovir ni dawa mojawapo ya ART jamii ya NtRTI inayotumika ikiwa imeungana na dawa zingine kudhibiti makali ya VVU.
Majina ya kibiashara
Tenofovir huuzwa katika jina jingine la Viread.
Ufanyaji kazi wa NtRTI
NtRTIs huzuia RNA ya kirusi kujitengeneza DNA yake, huweza kufanya hivyo kwa kuzuia kimeng’enya cha Reverse Transcriptase.
Dawa hii husaidia kupunguza VVU mwilini, kufanya ivi husaidia kinga ya mwili iweze kuongezeka.
Fomu ya Tenofovir
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na unga.
Unaweza tumia Tenofovir na chakula?
Hutumika pamoja na chakula ili iweze kufanya kazi vizuri.
Dawa zilizo kundi moja na Tenofovir
Dawa nyingine ambayo ipo kwenye kundi moja na Tenofovir(TDF) ni:
Tenofovir alafenamide (TAF)
Zidovudine (Retrovir)
Lamivudine (Epivir)
Abacavir sulfate (Ziagen)
Didanosine (Videx)
Stavudine (Zerit)
Emtricitabine (Emtriva)
Tenofovir hutibu nini?
Tenofovir hutumika pamoja na dawa zingine za kuthibiti VVU na kuzuia Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya mama kujifungua.
Hutumika kwa mgonjwa mwenye TB pamoja na HIV kama dawa ya kuthibiti HIV (ART) ambapo huchanganywa na Tenofovir , Efavirenz na kutengeneza mchanganyiko wa TLE
Hutumika kutibu homa sugu ya Ini kali inayosababishwa na kirusi cha hepataitizi B
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyoatakavyoelekezwa na Daktari
Dawa zilizo muunganiko na Tenofovir
Baadhi ya dawa zinazounganishwa na Tenofovir ili kuzuia kasi ya VVU ni;
Tenofovir (Tdf) +Lamivudine (3tc) + Dolutegravir (Dtg),
Tenofovir (Tdf)+Lamivudine (3tc) + Efavirenz (Efv)
Emtricitabine+Rilpivirine+Tenofovir Df
Emtricitabine+Tenofovir Af
Doravirine+Lamivudine+Tenofovir Df
Tenofovir disoproxil fumarate (Viread)
Lamivudine and zidovudine (Combivir)
Abacavir + lamivudine (Epzicom)
Abacavir+zidovudine + lamivudine (Trizivir)
Tenofovir disoproxil fumarate + emtricitabine (Truvada)
Tenofovir alafenamide + emtricitabine (Descovy)
Emtricitabine+Tenofovir+Efavirenz Df
Bictegravir+Emtricitabine+Tenofovir Af
Rilpivirine+Emtricitabine+Tenofovir Af
Darunavir+Cobicistat+Emtricitabine+Tenofovir Af
Wingiliano wa Tenofovir na dawa zingine
Tenofovir (TDF) haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Atazanavir
Amphotericin B
Tefenoquine
Streptozosin
Trimethropim
Bacitracin
Lasmiditan
Adefovir
Letermovir
Angalizo
Tenofovir inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa waliovimba ini.
Matumizi ya Tenofovir kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha haina madhara kwa mama mjamzito na mtoto
Matumizi ta Tenofovir kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote
Maudhi ya Tenofovir
Baadhi ya maudhi madogo ya Tenofovir ni;
Kukohoa
Chembechembe nyeupe za damu kupungua NJ
Misuli kuuma
Kichwa kuuma
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Tumbo kuuma
Je kama umeshau kutumia dozi yako ya Tenofovir ufanyaje ?
Tenofovir hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV endapo utasahau kutumia dozi yako, unapaswa tumia muda huo uliokumbuka na uendelea na muda huo siku inayofuata.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:23:00
Rejea za mada hii:-