Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Aprili 2020 13:10:08
Timolol
Timolol ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu kwenye mishipa ya damu na macho iliyo kwenye kundi la beta bloka.
Majina ya kibiashara
Timolol huuzwa kwa majina mengine ya kibiashara kama Blocadren
Fomu na uzito wa Timolol
Timolol pia hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
5mg
10mg na
20mg
Namna Timolol inavyofanya kazi
Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Timolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza presha kwenye macho
Hufanya kazi kwa kuzuia matendo ya kemikali mwilini kama epinefrini au beta adrenejik stimulesheni kwenye mishipa ya damu. Kwa kufanya hivi hupunguza presha kwenye macho
Dawa kundi moja na Timolol
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Acebutolol (Sectral)
Betaxolol (Kerlone)
Bisoprolol (Zebeta, Ziac)
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor)
Nebivolol (Bystolic)
Sotalol (Betapace)
Timolol hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye presha ya jicho
Hutumika kwenye matibabu ya glaucoma
Mwingiliano wa Timolol na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Xalatan
Vitamini C
Verapami
Synthroid
Sotalol
Saquinavir
Rivastigmine
Propranolol
Promethazine
Penbutolol
Omeprazole
Nebivolol
Nadolol
Mirtazapine
Milk of Magnesia
Metoprolol
Lofexidine
Lasix
Labetalol
Fiber Lax
Fentanyl
Esmolol
Diltiazem
Diltiazem
Digoxin
Clonidine
Celiprolol
Carvedilol
Brimonidine
Bisoprolol
Betaxolol
Benadryl
Aspirin
Artificial Tears
Aricept
Acidophilus
Acetaminophen
Acebutolol
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Timolol
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa jamii ya Beta bloka
Wagonjwa wenye asthma
Wagonjwa wenye bradikadia ya sainaz
Wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa moyo wa umeme
Wagonjwa wenye shoku ya kikadiojeniki
Wagonjwa wenye ugonjwa wa COPD
Matumizi ya Timolol kwa mama mjamzito
Timolol itumike kama faida ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kutokea kwa mtoto tumboni.
Matumizi ya Timolol kwa anayenyonyesha
Timolol imeonekana kuingia kwenye maziwa ya mama, mtoto anaweza kupatwa na madhara ya dawa kwa kunyonya maziwa ya mama anayetumia dawah ii. Kutokana na madhara ya mzio wa dawa, uamuzi unatakiwa kufanywa wa kuamua kuendelea au kuacha kutumia dawa hii wakati wa kunyonyesha.
Maudhi ya Timolol
Baadhi ya maudhi madogo ya Timolol ni;
Kuhisi kuungua kwenye macho
Kutokwa na mchozi kupita kiasi
Kuhisi mchanga machoni
Kuogopa mwanga
Kutoona vizuri wakati wa usiku
Je, kama umeshau dozi yako ufanyaje?
Kama umeshaau kutumia dozi yako ya Timolol, tumia mara pale utakapokumbuka. Endapo muda wa dozi umekaribia sana acha dozi uliyosahau kasha kusubiria muda wa dozi nyingine ili unywe dozi hiyo kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:23:07
Rejea za mada hii:-