Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020, 09:17:10
Tolazamide
Utangulizi
Tolazamide ni dawa inayotumika katika matibabu ya kisukari na Ipo kwenye kundi la kizazi cha kwanza cha dawa za sulfonylurea.
Fomula ya kikemikali
C14H21N3O3S
Majina mengine
• Tolinase
• Norglycin
• Tolanase
• Diabewas
• Tolazolamide
• Tolazamida
• Tolazamidum
Jina la kisayansi (IUPAC)
• 1-(azepan-1-yl)-3-(4-methylphenyl) sulfonylurea
Muonekakano
• Kidonge cheupe hakina hurufu kali, unaweza usihisi harufu yake pia.
Dozi inayopatikana
Kidonge kimoja kinaweza kuwa na:-
• 100mg
• 250mg
• 500mg
Jinsi ya kutumia
• Tumia kama utakavyo elekezwa na daktari wako
Maudhi madogo ya dawa
• Kushuka kwa Sukari
• Mzio kwenye ngozi
• Kiungulia
• Kizunguzungu
• Kichefuchefu
• Kutopata choo
• Kutapika
Maudhi makubwa
• Kushusha kiwango cha sukari kupita kiasi
• Manjano ya Ngozi na macho
• Sumu kwenye seli za ini (Kuua seli za Ini hivyo ini kushindwa kufanya kazi)
• Kupata degedege au kupoteza fahamu
Inafikaje kwenye damu?
• Inafyozwa upesi kutoka kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda kwenye damu baada ya kumezwa.
Inafanyaje kazi?
• Huchochea seli beta za kongosho kuzalisha homoni insulin ambayo hushusha sukari ya damu.
• Hupunguza kasi ya ini kutengeneza sukari.
• Inaongeza uwezo wa seli za mwili kupokea insulin hivyo kushusha sukari kwenye damu.
• Inaongeza idadi ya vipokezi vya insulin kwenye seli za mwili hivyo insulini kufanya kazi vizuri.
Mengine Zaidi yanayofanyika mwilini
• Huanza kufanya kazi dakika 20 baada ya kumeza.
• Hufanya kazi mwilini kati ya saa 14 hadi 24 baada ya kumeza.
• Uwezo wa kufanya kazi hufika kilele kati ya saa 4 hadi 6
• Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kupunguza sumu.
• Takamwiki ya mabaki yake hutolewa kwa njia ya mkojo( asilimia 85) na haja kubwa (asilimia 7)
Marufuku kwa wagonjwa wafuatao;
• Wenye mzio (allergy/aleji) na kemikali ya salfa.
• Wagonjwa wa sukari inatibika kwa insulini pekee (sukari aina ya kwanza).
• Wagonjwa ambao ini linashindwa kufanya kazi.
• Wagonjwa ambao figo ina shindwa kufanya kazi.
Tahadhari
• Chukua taadhari kwa wagonjwa wenye maambukizi ya magojwa mengine au homa.
• Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji au wenye majeraha.
• Huanza kufanya kazi upesi sana.
• Huweza kusababisha kukojoa mara kwa mara
Mungiliano na dawa nyngine:
Hatari ya kushusha sukari kupita kiasi endadapo itatumiwa na dawa nyingine za sukari kama vile:-
• Sulfonamides
• Propranolol
• Salicylates
• Phenylbutazone
• Probenecid
• Dicumarol
• Chloramphenicol
Dawa zifuata zinaweza kuongeza ufanjaji kazi wa tolzamide:-
• Clofibrate
• Halofenate
Tahadhari inahitjijaka ikiwa itatumika pamoja na isoniazid ambayo hutibu kifua kikuu.
Matumizi wakati wa ujauzito au kunonyesha
Ni vyema kuiepuka kwani bado haijajulkana kama inaweza kufika kwenye maziwa ya mama.
Kundi la dawa kwenye ujauzito
Dawa hii ipo kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 10:55:10
Rejea za mada hii:-