Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
19 Aprili 2020 12:05:56
Tolbutamide
Tolbutamide ni dawa ya kumeza inayotumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kisukari, iliyo kwenye kundi la sulphonylurea.
Majina ya kibiashara
Tolbutamide huuzwa kwa jina jingine la orinase
Tolbutamide na chakula
Anapaswa kuwa amekula wakati wa kumeza dawa, au anapaswa kutumia dawa Pamoja na chakula ili kuzuia kushuka kwa sukari kwenye damu.
Dawa kundi moja na Tolbutamide
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Tolbutamide ni;
Glibenese (Glipizide)
Minodiab (Glipizide)
Amaryl (Glimepiride)
Daonil (Gilbenclamide)
Chlorpropamide
Diamicron (Gilclazide)
Diamicron MR (Gilclazide)
Jinsi Tolbutamide inavyofanya kazi
Huchochea seli za Beta katika kongosho kuzalisha homoni ya Insulin
Hupunguza kiasi cha homoni ya glucagon kwenye damu
Hufanya kongosho kuitikia uzalishaji wa homoni ya insulin
Tolbutamide hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa kisukari aina ya pili
Mwingiliano wa Tolbutamide na dawa zingine
Tolbutamide haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Aminolevulinic acid oral
Erdafitinib
Ethanol
Ivosidenib
Lumacaftor
Methyl aminolevulinate
Siponimod
Wagonjwa waiopaswa kutumia Tolbutamide
Tolbutamide haipaswi kutumika kwa;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Wagonjwa wa dayabetiki ketoasidosisi
Kisukari cha aina ya kwanza
Angalizo la Tolbutamide
Inapaswa kusimamishwa kwa mgonjwa mwenye sukari ya chini
Dawa inaongeza hatari ya matatizo ya moyo
Kwa mgonjwa mwenye upungufu kimeng’enya cha glucose-6-phosphate dehydrogenase huweza kupata upungufu wa damu kutokana na kuvunjwa vunjwa kwa seli za damu
Matumizi ya Tolbutamide kwa mama mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Matumizi ya Tolbutamide kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Tolbutamide
Baadhi ya maudhi madogo ya Tolbutamide ni;
Sukari kushuka
Mwitikio wa disalfiramu
Upungufu wa seli nyeupe za damu(leukopenia)
Hyponatremia
Aplastiki anemia
Upungufu wa chembe sahani za damu(Thrombosaitopenia)
Kiungulia
Kichefuchefu
Kutapika
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje;
Kama umesahau dozi yako ya Tolbutamide, unaweza tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, ruka dozi uliyosahau mpaka ufike muda wa dozi nyingine kasha tumia dozi moja tu kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:23:21
Rejea za mada hii:-