Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Mei 2020 19:45:41
Triamterene
Triamterene ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic.
Majina ya kibiashara ya Triamterene
Triamterene huwa maarufu kwa jina la Dyrenium.
Fomu na dozi
Triamterene hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;
50 mg
100 mg
Ufanyaji kazi wa Triamterene
Dawa jamii ya Potassium Sparing Diuretic ikiwa pamoja na Triamterene hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;
Hufanya kazi kwa kuzuia utendaji kazi wa homoni ya Aldosterone ambayo hufanya kazi ya kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji kwenye damu. Kuzuia utendaji kazi wa homoni hii husababisha kupotea kwa maji na chumvi mwilini hivyo kupunguza kiwango cha damu katika mishipa ya damu na shinikizo la damu ndani ya mishipa pia hupungua kutokana na kupungua kiwango cha maji. Dawa hii pia huzuia kupotea kwa kiwango cha potasiamu kwenye damu, hii ndo maana jina la kundi hili limeitwa potasiamu sparing diuretics
Dawa kundi moja na Triamterene
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Amiloride
Spironolactone
Eplerenone
Triamterene hutibu nini?
Hutumika kupunguza uvimbe kwa wagonjwa waliovimba mwili kutokana kujaa kwa maji kwenye tishu
Hutumika katika matibabu ya shinikizo la juu la damu
Upekee wa Triamterene
Utofauti wa pekee wa Triamterene na dawa zingine za kwenye kundi lake ni kuchukua muda mfupi zaidi ili kuanza kutenda kazi ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili.
Muingiliano wa Triamterene na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amiloride
Drospironone
Eplerenone
Cyclosporine
Drospirenone
Lofexidine
Potassium acid phosphate
Potassium Chloride
Potassium citrate
Spironolactone
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Triamterene
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine katika kundi lake
Wagonjwa wenye Haipakalemia
Haipaswi kutolewa pamoja na dawa yeyote ya Potasiamu Sparing Diuretics
Wagonjwa wenye figo iliyoferi na magonjwa sugu ya ini
Angalizo
Tahadhari ya matumizi ya triamterene inapasw akuchukuliwa kwani
Huweza kupelekea kupoteza electrolaiti
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya ini na figo.
Matumizi ya Triamterene kwa mama mjamzito
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Matumizi ya Triamterene kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu huenekana kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Maudhi ya Triamterene
Baadhi ya maudhi madogo ya Triamterene ni;
Edema
Haipotension
Kizunguzungu
Kuchoka
Vipele
Kuharisha
Kutapika
Sumu kwenye figo
Kuishiwa pumzi
Umetaboli wa Triamterene
Dawa hii baada ya kutumiwa huanza kufanya kazi ndani ya saa 2 hadi 4 na kudumu kwenye damu kwa saa 12 hadi 16. Mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo.
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau dozi yako ya Triamterene tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau kisha endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-