Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Aprili 2020, 07:36:52

Voglibose
Voglibose ni ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kuhakikisha kinabaki kwenye kiwango cha kawaida kwa wagonjwa wenye kisukari. Dawa hii huzuia kiwango cha sukari ya damu kupanda kupita kiasi mara baada ya kula na hutumika pamoja na masharti ya kuzingatia mlo sahihi na mazoezi kwa wagonjwa wa kisukari.
Majina ya kibiashara
Jina la kibiashara la Voglibose ni Basen
Fomula ya kikemikali
Fomula ya kikemikali ya Voglibose ni C10H21NO7
Jina la kisayansi (IUPAC)
Jina la kisayansi la Voglibose ni (1S,2S,3R,4S,5S)-5-(1,3-dihydroxypropan-2-ylamino)-1- (hydroxymethyl)cyclohexane-1,2,3,4-tetrol
Namna ya kutumia Voglibose
Meza dawa hii kadri ulivyo elekezwa na daktari wako.
Meza dawa hii punde kabla ya kula.
Dawa hii huweza kutumiwa pamoja na dawa nyingine kama vile metformin, kama akipendekeza daktari wako.
Namna Voglibose inavyofanya kazi mwilini.
Dawa ya Voglibose huchelewesha mmeng'enyo wa vyakula vya wanga ili kuchelewesha kuzalisha sukari na hivyo huzuia kupanda kwa kiwango cha sukari kweenye damu mara baada ya kula.
Kwa kuchelewesha mmeng'enyo wa vyakula vya wanga, pia huchelewesha kufyonzwa kwa sukari kutoka kwenye mfumo wa chakula kwenda kwenye damu hivyo kuzuia kuongezeka kwa kiwango cha sukari ya damu mara baada ya kula.
Madhara madogo
Maudhi madogo ya Voglibose ni;
Maumivu ya tumbo
Tumbo kujaa hewa
Kujamba
Kuharisha
Vipele kwenye Ngozi
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Voglibose
Wenye mzio na dawa hii
Wagonjwa wa kisukari aina ya kwanza
Wagonjwa ambao figo zimeshindwa kufanya kazi
Wagonjwa waliowahi kupata dayabetiki ketoasidosisi (DKA)
Wagonjwa waliopata tatizo la kuziba kwa utumbo wa chakula.
Matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Ni vyema kuepuka kutumia dawa hii wakati wa ujauzito na kunyonyesha kwani hakuna taarifa/tafiti za kutosha kuhusu madhara ya dawah hii kwa mama au mtoto anaye nyonya.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:21:48
Rejea za mada hii:-