Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Aprili 2020 19:25:00
Zidovudine (AZT)
Zidovudine ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs.
Dawa hii haitumiki kama yenyewe, huchanganywa na dawa zingine za ART kudhibiti makali ya VVU.
Kundi la dawa za NRTIs hufanya kazi ya kupunguza makali ya VVU kwa kuzuia RNA ya kirusi kujitengenezea DNA. Ili RNA itengeneze DNA inahitaji kimeng’enya kinachoitwa Reverse Transcriptase, abacavir huzuia kimeng’enya hiki na hivyo kirusi kushindwa kujuzalia.
Fomu na uzito
Zidovudine hupatikana kwenye fomu ya kidonge, tembe na kimimnika cha kunywa. Uzito wa tembe na kidonge ni wa miligramu 100 au 300, dawa ya maji huwa na miligramu 50 kwa kila mililita tano za maji.
Majina ya kibiashara ya Zidovudine
Zidocudine hufahamika kwa jina jingine la kibiashara kama azidothymidine
Je Zidovudine inaweza kutumika na chakula?
Huweza kutumika pamoja na chakula lakini chakula hicho kisiwe chenye mafuta sana
Dawa zilizo kundi moja na Zidovudine
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na zidovudine ni zifuatazo:
Lamivudine (3TC)
Emtricitabine (FTC)
Abacavir (ABC)
Zidovudine hutibu nini?
Kazi za zidovudine (AZT) ni kama zifuatazo:
Hutumika kama muunganiko wa kwanza katika kuthibiti virusi vya HIV pamoja na muunganiko wa dawa zifuatazo ;
Lamivudine (Epivir)
Abacavir sulfate (Ziagen)
Didanosine (Videx)
Didanosine (Videx EC)
Stavudine (Zerit)
Emtricitabine (Emtriva)
Tenofovir disoproxil fumarate (Viread)
Hutolewa pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV kuzuia Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya mama kujifungua,Mama anapaswa kunywa bila kuruka ruka dozi
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na Daktari
Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Zidovudine
Zidovudine haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Emtricitabine
Ganciclovir
Ribavirin
Abacavir
Clozapine
Clarithromycin
Atanazavir
Ketokonazole
Methotrexate
Mitomycin
Rifampin
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Zidovudine
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye chembe za Neutrophils kidogo kwenye damu
Wenye upungufu wa damu
Wenye Ini lililoferi
Angalizo kwa watumiaji wa Zidovudine
Inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye hatari ya kupungukiwa damu
Wenye uzito kupita kiasi(obeziti)
Magonjwa mengine yanayoharibu kinga ya mwili kama ugonjwa wa Graves
Matumizi ya Zidovudine kwa mama mjamzito
Hutumika kwa mama mjamzito kwa ajili ya kuzuia na kupunguza Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hivyo matokeo ya dawa hukabiliwa na kuthibitiwa kwa shida yeyote itakayojitokeza
Matumizi ya Zidovudine kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote
Maudhi ya Zidovudine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:
Uchovu mkali wa mwili
Kuwa na homa
Kushuka kwa chembechembe nyeupe za damu
Maumivu ya misuli
Kuchoka
Maumivu ya kichwa
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Upungufu wa damu
Konstipesheni
Kukosa usingizi
Je endapo utasahau dozi yako ya Zidovudine ufanyaje ?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti VVU, endapo utasahau kutumia dozi yako, unapaswa tumia na Kuendelea na muda huo siku inayofuata kama ulivyoshauriwa na daktari wako
Lakini ukikumbuka kunywa baada ya masaa 24 kupita, kunywa dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari na achana na dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:21:46
Rejea za mada hii:-