top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

14 Aprili 2020 05:29:18

Ziprasidone

Ziprasidone

Ni dawa mojawapo ya kizazi cha pili katika kundi la dawa antisaikotiki (kundi hili hufahamika pia kama atipiko antisaikotiki )


Dawa hii huwa na maudhi kidogo kulinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili, pia huwa na uwezo sawa na dawa za antisaikotiki kizazi cha kwanza.


Rangi na Fomu ya Ziprasidone


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa tembe


Jina la kibiashara la ziprasidone


Dawa hii huuzwa katika jina la Geodon


Matumizi na chakula


Ziprasidone hutumika baada ya kula chakula


Dawa zilizo kundi moja na Ziprasidone


  • Quetiapine

  • Olanzipine

  • Aripiprazole


Jinsi Ziprasidone inavyofanya kazi


Hufanya kazi kwa kufunga na kuzuia receptor za dopamine na serotonin na kuzuia utendaji kazi wao kwa wingi sababu , neurotransmitter hizi huthibiti hali ya mawazo ,hisia na tabia


Ziprasidone hufanya kazi kwa kuziba risepta za homoni ya serotonin-2A na dopamine D2 kama dawa zingine za antisaikotiki ya atipiko, hata hivyo utofauti wake ni kwamba ina uwezo mkubwa Zaidi wa kuziba njia za risepta hizi 2A/D2 ukilinganisha na dawa zingine za antisaikotiki kama 5- olanzapine, quetiapine, risperidone, na aripiprazole.


Njia hizi zinzpozibwa homoni asili za seroton na dopamine hushindwa kufanya kazi yake. Soma Zaidi kuhusu kazi za homoni hizi kwenye Makala za homoni.


Ziprasidone hutibu nini?


  • Hutumika kutibu ugonjwa wa schizofrenia

  • Hutumika kutibu ugonjwa wa baipola mania

  • Hutumika kutibu wasiwasi na woga uliopitiliza


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Ziprasidone


  • Amiodarone

  • Amoxapine

  • Arsenic trioxide

  • Citalopram

  • Disopyramide

  • Escitalopram

  • Goserelin

  • Ibutilide

  • Indapamide

  • Leuprolide

  • Pentamidine

  • Pimozide

  • Procainamide

  • Quinidine

  • Saquinavir

  • Sorafenib

  • Sotalol

  • Toremifene


Angalizo kwa watumiaji wa ziprasidone


  • Huweza kupelekea kupungua kwa chembechembe nyeupe za damu

  • Kuongezeka kwa sukari mwilini

  • Huweza kuathiri uwezo wa mtu kusimama kwa muda mrefu na kumpelekea kuanguka

  • Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye mzio na dawa hii na mwenye shida ya moyo


Matumizi ya Ziprasidone Kwa mama mjamzito


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito.


Matumizi ya Ziprasidone Kwa mama anayenyonyesha


Kwa mama anayenyonyesha haipaswi kutumika kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama


Maudhi ya Ziprasidone


  • Kulala kupita kiasi

  • Kuwa na woga na wasiwasi

  • MAumivu ya kichwa

  • Vipele

  • Kuchoka

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi

  • Kukohoa

  • Rinaitizi

  • Choo kigumu/konstipesheni

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya tumbo

  • Vipele

  • Kuhisi maigo ya moyo

  • Midomo kuwa mikavu

  • Kukosa hamu ya kula

  • Maumivu ya misuli

  • Kuongezeka uzito


Je endapo umesahau dozi ya Ziprasidone ufanyeje?


Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dozi anapaswa kuitumia pale atakapokumbuka

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:21:38

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman’s The pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 Ukurasa wa 418-435.Imechukuliwa 13/4/2020

2.WebMd.Ziprasidone.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-20568/ziprasidone-oral/details. Imechukuliwa 13/4/2020

3.DrugBank.Ziprasidone.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00246. Imechukuliwa 13/4/2020

4.Medscape.Geodon.https://reference.medscape.com/drug/geodon-ziprasidone-342985. Imechukuliwa 13/4/2020

5.MedlinePlus.Ziprasidone.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a699062.html. Imechukuliwa 13/4/2020
bottom of page