top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Peter A, MD

22 Novemba 2021, 18:59:55

Image-empty-state.png

Wiki ya 3 ya ujauzito

Hii ni wiki ambayo uchavushaji wa yai na utungishaji mimba hufanyika. Yai litarutubishwa na moja ya manii iliyomwagwa ukeni wakati wa ngono na kufanikiwa kupita kwenye shingo ya kizazi hadi kwenye mrija wa falopio ili kukutana na yai kisha kuingia ndani yake.


Mabadiliko yanayotokea


Mara baada ya yai kuchavushwa na manii, chembe mithiri ya mpira huanza kukua kwa nje huku ikigawanyika ndani kuwa chembe nyingi ndani yake. Katika hatua hii, matokeo ya uchavushaji yai hutengeneza blastosait, ambayo huwa na shemu mbili, sehemu ya nje ambayo itakuwa kondo la nyuma na sehemu ya ndani ambayo itakuwa kiini tete.

Wiki ya 3 ya ujauzito


Jinsia ya mtoto wako huamriwa wakati huu wa uchavushaji. Kwenye hatua hii Mtoto hufahamika kama kiinitete ambacho huwa na takribani chembe 150 zitakazokuwa kwenye matabaka mbalimbali yaliyoelezewa hapa chini.


Tabaka la ndani

Tabaka la ndani hufahamika kama endodem au endoblasti, hubadilika mbeleni na kutengeneza;


  • Njia ya hewa ya mfumo wa upumuaji

  • Mfumo wa umeng’enyaji chakula

  • Kongosho

  • Thyroid

  • Ini

  • Thymus


Tabaka la kati

Tabaka la kati hufahamika kama mesoderm, tabaka hili hukua na kutengeneza viungo vifuatavyo;

  • Mifupa

  • Misuli

  • Moyo na mishipa ya damu

  • Mfumo wa utoaji taka mwilini

  • Maumbile ya kike na kiume


Tabaka la nje

Tabaka la nje hufahamika pia kama ektodem au ektoblast. Hukua na kuengeneza viungo vifuatavyo;

  • Ubongo

  • Ngozi

  • Kucha

  • Nywele


Wakati kiinitete kinapata mabadiliko haya, huwa kinaelea ndani ya tumbo la uzazi kikiwa kinalindwa na ute ute unaozalishwa na kizazi.


Unaweza kuona kijusi kwa ultrasound?


Endapo kipimo cha ultrasound kitafanyika wakati huu, hakitakuwa na uwezo w akuonyesha kiinitete wakati huu kwa macho ya nyama.


Mambo mengine unayotakiwa kuyaangalia


Kama umekuwa ukipima joto la mwili wako, joto la mwili wakati wa asubuhi kabla ya kutoka kitandani au kabla ya kufanya kazi yoyote ile, utaona kwamba limekuwa kubwa hata baada ya siku ya 16 tangu uovuleshaji umetokea. Hii ni ishara ya kwanza ya kifiziolojia ya kuwa una ujauzito.


Mambo muuhimu unaweza fanya katika hatua hii ni kuachana na matendo yanayohatarisha afya na uumbaji wa mtoto kama vile;


  • Kuvuta sigara

  • Kunywa pombe

  • Kutumia dawa za kulevya


Kufanya hivi ni jambo jema kwa afya yako, ya ujauzito, na kujifungua.


Virutubisho vya nyongeza


Kipindi hiki ni maalumu kuanza kufikiria kuhusu matumizi ya virutubisho vya nyongeza ikiwa pamoja na vitamin na madini.


Unashauriwa kupata angalau mikrogramu 400 za folic acid, vitamin B9 ushauriwa kutumika ili kupunguza hatari ya mtoto kupata madhaifu ya kuzaliwa mfano mgongo wazi na ubongo wazi.


Folic acid huwa na faida nyingi kwa mtoto ambazo ni;

  • Husaidia mwili kutengeneza protini mpya

  • Husaidia mwili kutengeneza chembe nyekundu za damu

  • Hukinga mtoto kuzaliwa na mgongo wazi

  • Hukinga mtoto kuzaliwa na ubongo wazi


Soma zaidi kuhusu folic acid kwenye ujauzito hapa


Majina mengine


Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:

  • Ujauzito wa wiki 3

  • Mimba ya wiki 3

  • Wiki 3 ya mimba

  • Kijusi cha wiki 3

  • Mwonekano wa ujauzito wa wiki 3

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

12 Julai 2022, 10:22:12

Rejea za dawa

  1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

  2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

  3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

  4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

  5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

  6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

  7. Kagan KO, et al. Principles of first trimester screening in the age of non-invasive prenatal diagnosis: screening for chromosomal abnormalities. Arch Gynecol Obstet. 2017 Oct;296(4):645-651. [PubMed]

  8. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

  9. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

  10. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page