top of page

Folic acid kwa mjamzito

Updated: Sep 16, 2021

Folic acid ni nini?


Folic acid ni aina ya vitamin B inayopatikana katika vyakula mbalimbali tunavyokula kila siku kama mkate, mboga za majani n.k. Licha ya kupatikana kwenye mvyakula, kuna baadhi ya watu wanatakiwa tumia vitamin hii nyongeza kutoka kwenye vidonge kutokana na ongezeko la mahitaji, mfano kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Wakati gani sahihi wa kuanza kutumia folic acid kwa mjamzito?


Inashauriwa kitalaamu kuanza kutumia vidonge vya folic acid unapopanga kuwa mjamzito yaani angalau mwezi mmoja kabla ya kupata ujauzito ili kuufanya mwili wako uzalishe seli mpya.


Unaweza kunywa folic acid kila siku kabla ya kuwa mjamzito na mpaka ukafikisha wiki ya 12 ya ujauzito.


Endapo hujaanza kutumia vidonge kabla hujapata mimba, unatakiwa kuanza kutumia mara tu utakapogundua kuwa una ujauzito.


Folic acid huwa na muhimu gani kwa kijusi tumboni?


Folic acid huzuia husaidia utengenezaji wa mfumo wa fahamu wa kijusi na hivyo huzuia ulemavu wa mfumo wa fahamu mfano tatizo la mgongo wazi linalofahamika kama spina bifida na anaensefal linalofahamika kama ubongo wazi


Umuhimu mwingine ambao umeonekana kwenye tafiti ni kuzuia ulemavu wa moyo


Naweza kupata madini ya folic acid ya kutosha kutoka kwenye chakula tu bila kutumia kidonge?


Hapana!


Licha ya kuwa na vyakula vingi vyenye madini ya folic acid kama mboga za kijani na mbegu za mimea mbalimbali, mama mjamzito kwa kuwa anamahitaji makubwa ya vitamin hii, ni vigumu kupata kiasi kinachoshauriwa kwa siku kutoka kwenye vyakula tu.Ni dozi gani ya folic acid mjamzito anatakiwa kutumia kwa siku?


Mama anatakiwa kutumia kila siku mikrogramu 400 za kidonge cha folic acid.


Wakati gani mjamzito anahitaji dozi kubwa ya folic acid?


Endapo una kihatarishi cha kupata mtoto mwenye mgongo wazi, utashauriwa kutumia dozi kubwa zaidi ya folic acid kila siku mpaka ujauzito utakapofikisha wiki 12.


Vihatarishi vya kupata mtoto mwenye mgongo wazi ni vipi?


Endapo una kihatarishi cha kupata mtoto mwenye mgongo wazi, ni vema ukawasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi wa dozi gani ya folic acid utumie. Baadhi ya vihatarishi vya kupata mtoto mwenye mgongo wazi ni;

 • Baba wa mtoto kuwa na tatizo la mgongo wazi

 • Ndugu wa damu wa baba ya mtoto ana tatizo la mgongo wazi

 • Ulishakuwa na ujauzito uliopita wa mtoto mwenye mgongo wazi

 • Unaugonjwa wa kisukari

 • Unatumia dawa za kutibu kifafa

 • Unatumia ARV kwa matibabu ya VVU/UKIMWI


Wakati gani wa kuacha kutumia folic acid wakati wa ujauzito?


Mfumo wa fahamu huwa umeshatengenezwa mpaka kufikia wiki12 za mwanzo wa ujauzito. Baada ya wiki hizi mama anaweza kuacha kutumia madini hayo au kuedelea nayo endapo atapenda.


Kuna madhara kwa mama na mtoto ya kuendelea kutumia folic acid baada ya wiki 12 za ujauzito kupita?


Kuendelea kutumia madini ya folic acid baada ya wiki 12 za kwanza za ujauzito imeonekana kusaidia kuimarisha ufahamu wa watoto. Kwa maana hiyo hakuna madhara ya kutumia madini haya hata baada ya wiki 12 za ujauzito


Rejea za mada hii


 1. Mary Wanjira Kamau, et al. Effect of a community-based approach of iron and folic acid supplementation on compliance by pregnant women in Kiambu County, Kenya: A quasi-experimental study. https://journals.plos.org/plosone/article?id=10.1371/journal.pone.0227351. Imechukuliwa 24.06.2021

 2. James A Greenberg, MD, et al. Folic Acid Supplementation and Pregnancy: More Than Just Neural Tube Defect Prevention. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3218540/. Imechukuliwa 24.06.2021

 3. Folic acid. https://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-1017/folic-acid. Imechukuliwa 24.06.2021

 4. CDC. Folic acid. https://www.cdc.gov/ncbddd/folicacid/about.html. Imechukuliwa 24.06.2021

 5. Rieder MJ. Prevention of neural tube defects with periconceptional folic acid. Clin Perinatol. 1994;21:483–503.

 6. Pitkin RM. Folate and neural tube defects. Am J Clin Nutr. 2007;85:285S–288S.

 7. De Wals P, et al. Reduction in neural-tube defects after folic acid fortification in Canada. N Engl J Med. 2007;357:135–142.

 8. Helene McNulty, et al.

 9. Effect of continued folic acid supplementation beyond the first trimester of pregnancy on cognitive performance in the child: a follow-up study from a randomized controlled trial (FASSTT Offspring Trial). https://bmcmedicine.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12916-019-1432-4. Imechukuliwa 24.06.2021

1,572 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page