Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
Jumanne, 5 Mei 2020

Faida za Viazi vitamu
Viazi vitamu ni chakula cha mzizi kinacholimwa ardhini, viazi vina sifa ya utamu. Wanasayansi wamegundua kuwa viazi vitamu ni chanzo kizuri cha Vitamin A na vitamin B5, niacin, Riboflavin,na thiamine
Pia tafiti zinaonyesha kuwa kula viazi vitamu vinaweza kuzuia hali ya kuvimba mwili, saratani na kisukari
Faida za viazi vitamu
Husaidia mwili kutokuwa na upungufu wa vitamin A na hivyo kupambana na magonjwa ya macho
Huwa na wingi wa Madini ya Magnesium ambayo husaidia katika kuthibiti hali ya msongo wa mawazo na hali ya huzuni
Kemikali za choline na anthocyanins huzuia mwili kuvimba
Husaidia kukinga na kuthibiti saratani, pia huwa na carotene ambayo huzuia Wanaume wasipate saratani ya tezi dume
Husaidia kidonda kupona kwa haraka
Majani ya viazi vitamu yana polyphenols ambayo husaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo
Majani ya viazi vitamu yana ethanol na acetone ambayo ina hali ya uwezo wa kupambana na bakteria mwilini
Viazi vitamu vina wingi wa vitamin A na majani wingi wa Vitamin E ambayo husaidia uimara wa nywele
Husaidia kurahisisha umeng’enyaji wa chakula
Kutokana na uwepo wa magneziamu na potassiamu husaidia kushusha shinikizo la damu
Husaidia mtu kuona vizuri kutokana na kuwa na Vitamin A
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:12:03
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Health Line Sweet Potatoes https://www.healthline.com/nutrition/sweet-potato-benefits. Imechukuliwa 11/4/2020
Good For food Benefits of sweet potatoes https://www.bbcgoodfood.com/howto/guide/health-benefits-sweet-potato. Imechukuliwa 11/4/2020
FOOD REVOLUTION SWEET POTATOES https://foodrevolution.org/blog/sweet-potato-health-benefits/amp/. Imechukuliwa 11/4/2020
Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 261. Imechukuliwa 11/4/2020