Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, C.O
Dkt. Benjamin L, M.D
Ijumaa, 28 Januari 2022
Tini
Tini ni matunda madogo yanayotokana na miti midogo ya maua kutoka kundi la Ficus carica na familia ya Moraceae. Tini inakua imesheheni virutubisho na vitamini kwa wingi kuwezesha ujenzi wa mwili, kurekebisha sukari n.k
Viinirishe vinavyopatikana kwenye Tini
Mafuta
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Protini
Sukari
Madini
Vitamini
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Tini
Tunda la Tini lina kemikali muhimu inayoitwa Cyanidin
Viinirishe vinavyopatikana kwenye Tini
Nishati = 74kcl
Jumla ya mafuta = 0.1g
Sukari = 16g
Nyuzilishe = 2.4g
Protini = 0.3g
Kabohaidreti = 19mg
Maji = 79.11g
Madini yanayopatikana kwenye Tini Zenye Gramu 100
Chuma = 0.37mg
Kalisiamu = 35mg
Magneziam = 17mg
Fosifolasi = 14mg
Potasiamu = 232mg
Sodiamu = 1mg
Manganizi = 0.128mg
Zinki = 0.15mg
Vitamini zinazopatikana kwenye Tini zenye gramu 100
Vitamin A = 7mcg
Vitamini B1 = 0.06mg
Vitamini B2 = 0.05mg
Vitamini B3 = 0.4mg
Vitamini B5 = 0.5mg
Vitamini B6 =0.113mg
Vitamini B9 = 6mcg
Vitamini C = 2mg
Vitamini E = 0.11mg
Vitamini K = 4.7mcg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Tini
Huimarisha mfumo mzima wa mishipa ya damu, hivyo kuzuia shinikizo la juu la damu.
Huimarisha kinga ya mwili na kuzuia saratani za aina mbalimbali.
Huimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Huimarisha utendaji kazi wa mfumo wa fahamu.
Huimarisha afya ya ngozi
Hutibu kikohozi
Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo ni sahihi kutumiwa na wagonjwa kisukari
Hutibu na kuzuia tatizo la kuharisha
Hutibu na kuzuia minyoo tumboni
Imeboreshwa,
28 Januari 2022, 08:14:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Figs nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Figs%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g&utm_source=share-by-url. Imechukuliwa 27/12/2021
Subash S, Essa MM, Braidy N, Al-Jabri A, Vaishnav R, Al-Adawi S, Al-Asmi A, Guillemin GJ. Consumption of fig fruits grown in Oman can improve memory, anxiety, and learning skills in a transgenic mice model of Alzheimer's disease. Nutr Neurosci. 2016 Dec;19(10):475-483. doi:10.1179/1476830514Y.0000000131. Epub 2016 Mar 2. PMID: 24938828. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24938828/. Imechukuliwa 27.12. 2021.
Solomon A, Golubowicz S, Yablowicz Z, et al. Antioxidant activities and anthocyanin content of fresh fruits of common fig (Ficus carica L.) Journal of Agricultural and Food Chemistry. 2006;54(20):7717–7723. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3789402/. Imechukuliwa 27.12.2021.
